Israel yazuia wakaguzi wa UN kuchunguza mateso katika jela zake
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekaidi matakwa ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguzwa mateso wanayoyapata Wapalestina katika jela za utawala huo dhalimu.
Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Michal Sarig-Kaduri amedai kuwa kuna vitendo vichache sana vya mateso ya wafungwa katika jela za utawala huo.
Siku ya Jumanne, Kamati ya kupambana na utesaji ya Umoja wa Mataifa ilitazamiwa kuwahoji maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na sera za utawala huo za kuwatesa wafungwa wa Kipalestina.
Kamati hiyo ya kupambana na utesaji ya UN ilitazamiwa kuwafanyia usaili maafisa hao wa utawala ghasibu wa Kizayuni kwa muda wa siku mbili kuanzia siku ya Jumanne na kuendelea hadi jana kuhusiana na sera zao za kuwatesa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo. Utawala wa Kizayuni wa Israel umesaini Mkataba wa mwaka 1991 wa Umoja wa Mataifa unaopiga marufuku utesaji wafungwa.
Ubomoaji wa nyumba za Wapalestina, ukatili wanaofanyiwa Wapalestina na walowezi wa Kizayuni na jinsi utawala haramu wa Israel unavyoshughulikia malalamiko yanayohusiana na utesaji, ni masuali mengine ambayo maafisa wa utawala huo ghasibu watapaswa kuyatolea majibu mbele ya kamati ya kupambana na utesaji ya Umoja wa Mataifa.