Hamas: Serikali za Marekani daima huukingia kifua utawala haramu wa Israel.
(last modified Mon, 09 Nov 2020 08:22:32 GMT )
Nov 09, 2020 08:22 UTC
  • Hamas: Serikali za Marekani daima huukingia kifua utawala haramu wa Israel.

Mjumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa siasa za mambo ya nje za serikali zote zilizotawala Marekani daima zimekuwa zikiunga mkono na kuukingia kifua utawala haramu wa Israel

Ismail Ridhwan amesema kuwa harakati ya Hamas haina matarajio yoyote kwa rais mteule wa Marekani, Joe Biden na wala haina imani naye.

Ridhwan ameongeza kuwa, rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump ndiye kiongozi mbaya zaidi wa Marekani aliyeamiliana na kadhia ya Palestina na eneo zima la Magharibi mwa Asia kwa mieneno mibaya kupita yote. 

Mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Hamas ametilia mkazo suala la kusitishwa mara moja utekelezaji wa mpango wa Muamala wa Karne na njama ya kutaka kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Vilevile amezitaka nchi za Kiarabu ziache kusalimu amri na kuanzisha uhusiano na utawala huo ghasibu.  

Afisa huyo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina amesema kuwa Wapalestina wanapaswa kutegemea uwezo wao wa ndani kwa ajili ya kuanzisha umoja na mshikamano ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile iliyopachikwa jina la Muamala wa Karne.

Mpango huo uliobuniwa na Rais Donald Trump unaunaupa utawala haramu wa Israel eneo lote la Quds tukufu na kuwazuia wakimbizi wa Kipalestina walioko nje ya nchi kurejea katika nchi yao..   

Tags