Ndege za kivita za Israel zashambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64640-ndege_za_kivita_za_israel_zashambulia_kwa_mabomu_ukanda_wa_gaza
Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimeshambulia ngome za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Gaza mapema leo Jumapili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 15, 2020 08:30 UTC
  • Ndege za kivita za Israel zashambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza

Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimeshambulia ngome za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Gaza mapema leo Jumapili.

Mashambulizi hayo ya anga yamekuja masaa machache baada ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni kudai kuwa, jana usiku maroketi mawili yalivurumishwa kutoka Gaza na kudondoka kusini mwa ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.

Duru za kiusalama katika Ukanda wa Gaza zinaarifu kuwa, tokea jana usiku, ndege za kijeshi za utawala pandikizi wa Israel zimekuwa zikishambulia kwa mabomu miji ya Khan Younes, Rafah na Beit Hanoun katika ukanda huo.

Hata hivyo hakuna habari zozoteza za majeruhi au wahanga wa mashambulizi hayo ya Wazayuni zilizoripotiwa hadi sasa.

Mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Wapalestina wanne waliuawa shahidi baada ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia kwa mabomu maeneo kadhaa ya Palestina huko mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Eneo la Ukanda wa Gaza mbali na kushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya jeshi katili la Israel, kwa zaidi ya miaka 14 sasa limekuwa chini ya mzingiro wa anga, baharini na nchi kavu unaotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel.