HAMAS yaonya kuhusu kuendelea mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64792-hamas_yaonya_kuhusu_kuendelea_mzingiro_dhidi_ya_ukanda_wa_gaza
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusiana na matokeo mabaya ya kuendeleza mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza sambamba na kushadidishwa hujuma na mashambulio dhidi ya eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 23, 2020 04:43 UTC
  • HAMAS yaonya kuhusu kuendelea mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusiana na matokeo mabaya ya kuendeleza mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza sambamba na kushadidishwa hujuma na mashambulio dhidi ya eneo hilo.

Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, utawala dhalimu wa Israel unafuta visingizio kwa ajili ya kudumisha mzingiro na mashambulio yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, hii kwamba, daima Israel imekuwa ikiionyeshea kidole cha lawama harakati hiyo na kuitaja kuwa ndio inayobeba dhima ya matukio ya Gaza, ni utafutaji visingizio tu vya kudumisha mzingiro na mashambulio ya jeshi lake dhidi ya eneo hilo ambalo ni nembo halisi ya muqwama na kusimama kidete.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unalizingira eneo la Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2006 wakati Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ilipoibuka na ushindi katika uchaguzi wa Bunge la Palestina.

Wanawake na watoto nd wahanga wakuu wa hujuma na mashambulio ya utawala vamizi wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza

 

Tangu wakati huo Israel imekuwa ikizuia kuingizwa bidhaa zote muhimu katika eneo hilo kama vile chakula, dawa, vifaa vya ujenzi na kadhalika na kulifanya eneo hilo kukabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu. 

Hivi sasa wakazi wa Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na mashaka na matatizo makubwa kwa ajili ya kupata huduma muhimu kama dawa, maji na chakula, huku asasi mbalimbali za kieneo na kimataifa zikitahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea maafa ya kibinadamu katika eneo hilo.