Ansarullah Yemen: Marekani chanzo kikuu cha mauaji ya wananchi wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65093-ansarullah_yemen_marekani_chanzo_kikuu_cha_mauaji_ya_wananchi_wa_yemen
Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha jinai zinazofanywa na Saudi Arbia dhidi ya watu wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 09, 2020 04:41 UTC
  • Ansarullah Yemen: Marekani chanzo kikuu cha mauaji ya wananchi wa Yemen

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha jinai zinazofanywa na Saudi Arbia dhidi ya watu wa Yemen.

Muhammad Ali al Houthi ameandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba:  Marekani imeziruhusu Saudi Arabia na waitifaki wake kuwauwa wananchi wa Yemen kwa kupokea fedha kutoka kwa nchi za Kiarabu zilizoivamia nchi hiyo. 

Muhammad Ali al Houthi amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani ameuwa wananchi wa Yemen ikiwa ni katika kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba atapunguza idadi ya watu wasio na ajira na kulipa madeni. Ameongeza kuwa:  Marekani imefanikisha ahadi zake hizo na njama nyingine za Israel katika eneo hili kwa kupokea fedha kutoka kwa nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi.  

Rais Donald Trump wa Marekani  

Saudi Arabia huku ikungwa mkono na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Machi 25 mwaka 2015 zilianzisha hujuma na mashambulizi makubwa huko Yemen na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, angani na nchi kavu. 

Vita hivyo vya kidhulma vya Saudia na waitifaki wake huko Yemen hadi sasa vimesababisha kuuliwa Wayemeni zaidi ya elfu 16, kujeruhiwa makumi ya maelfu na kuwa wakimbizi mamilioni ya wengine.