Jeshi la Syria lakamata silaha za Israel mikononi mwa magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65197-jeshi_la_syria_lakamata_silaha_za_israel_mikononi_mwa_magaidi
Jeshi la Syria limekamata kiwango kikubwa cha silaha za kila namna za utawala wa Kizayuni wa Israel zilizokuwa zinatumiwa na magenge ya kigaidi kufanya jinai dhidi ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 15, 2020 02:30 UTC
  • Jeshi la Syria lakamata silaha za Israel mikononi mwa magaidi

Jeshi la Syria limekamata kiwango kikubwa cha silaha za kila namna za utawala wa Kizayuni wa Israel zilizokuwa zinatumiwa na magenge ya kigaidi kufanya jinai dhidi ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Shirika la habari la SANA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, jana Jumatatu, jeshi la Syria lilikamada idadi kubwa ya silaha tofauti zilizotengenezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel, kusini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, miongoni mwa silaha hizo za utawala wa Kizayuni zilizokamatwa na jeshi la Syria mikononi mwa magaidi ni AK-47, bunduki za rashasha nzito na nyepesi, bunduki maalumu za watunga shabaha kutokea mbali, RPG, aina kwa aina ya maroketi, ndege zisizo na rubani, silaha za kupiga kwa kuweka mabegani na aina nyingine mbalimbali za silaha ambazo zilikuwa zinatumiwa na magaidi kufanya jinai dhidi ya raia na maafisa wa serikali ya Syria.

Jeshila Syria likifurahia ushindi

 

Televisheni ya Syria imetangaza mara chungu nzima habari za kukamatwa silaha na zana za kivita za madola mbalimbali ya kibeberu hasa Israel, mikononi mwa magenge ya kigaidi.

Kiwango kikubwa zaidi cha silaha zilizowahi kukamatwa na jeshi la Syria kusini mwa nchi hiyo, ni zile zilizochukuliwa ngawira na jeshi hilo mwezi Aprili 2018 katika ghala za silaha la genge la kigaidi la "Jeysh al Islam" katika eneo la Qalamoun. Silaha hizo zilijumuisha makombora ya ardhi kwa ardhi, vifaru, makombora ya ardhi kwa anga, ndege zisizo na rubani, silaha za kurushia maroketi na silaha nyingine nyingi ambazo nyingi zake zimetengenezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.