HRW: Saudia inatumia mabomu ya vishada ya Marekani nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i6550-hrw_saudia_inatumia_mabomu_ya_vishada_ya_marekani_nchini_yemen
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeikosoa Marekani kwa kuiuzia Saudi Arabia mabomu ya vishada yanayotumiwa na utawala huo wa kifalme dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 06, 2016 23:49 UTC
  • HRW: Saudia inatumia mabomu ya vishada ya Marekani nchini Yemen

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeikosoa Marekani kwa kuiuzia Saudi Arabia mabomu ya vishada yanayotumiwa na utawala huo wa kifalme dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.

Steve Goose, Mkurugenzi wa Kitengo cha Silaha cha shirika hilo ameitaka serikali ya Washington kusimamisha uzalishaji na uuzaji wa mabomu ya vishada kinyume na sheria za kimataifa huku akiutaka utawala wa Aal-Saud kukoma kutumia mabomu hayo haramu dhidi ya raia wasio na hatia nchini Yemen. Goose amesema inasikitisha kuona mabomu hayo yanaendelea kutumiwa nchini Yemen licha ya taathira zake hasi haswa dhidi ya idadi kubwa ya raia huku akiitaka Marekani kutoyatengeneza na kutoyauza mabomu hayo haramu kwa nchi yeyote ile. Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu ni miongoni mwa nchin zilizonunua mabomu ya vishada kutoka Marekani katika miaka ya hivi karibuni.

Hadi sasa watu wasiopungua 9,400 wameshauawa na wengine zaidi ya 16,000 wamejeruhiwa tangu Saudia na washirika wake walipoanzisha mashambulio na uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la eti kumrejesha madarakani kibaraka wa utawala wa Aal Saud, Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi. Mashambulio hayo yameangamiza na kusababisha hasara kubwa kwa miundombinu ya Yemen, mbali na kulenga na kubomoa hospitali, shule, misikiti na turathi za kihistoria za nchi hiyo.