Kasisi mmoja Mzayuni akumbwa na kashfa ya fedha, maadili
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i6952-kasisi_mmoja_mzayuni_akumbwa_na_kashfa_ya_fedha_maadili
Kasisi mmoja Mzayuni ambaye ni mtu wa karibu sana na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekumbwa na kashfa za fedha na maadili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 12, 2016 23:40 UTC
  • Kasisi mmoja Mzayuni akumbwa na kashfa ya fedha, maadili

Kasisi mmoja Mzayuni ambaye ni mtu wa karibu sana na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekumbwa na kashfa za fedha na maadili.

Televisheni ya al Mayadeen imetangaza habari hiyo na kuwanukuu Wakristo wa mji wa Quds wakitaka kasisi Gabriel Nadaf avuliwe nguo za uchungaji kutokana na kukumbwa na kashfa za ufisadi wa kifedha na kimaadili.

Askofu Atallah Hanna, mkuu wa maaskofu wa Orthodox katika mji wa Quds amesema, kama tuhuma zinazomkabili kasisi huyo zitadhibitika, itabidi avuliwe mavazi ya uchungaji kwani kanisa lao linafundisha kuwa pamoja na wanyonge na wanaodhulumiwa na kusimama kidete kukabiliana na madhalimu. Hivyo mtu yeyote anayemsaidia dhalimu kutenda dhulma zake, huyo ni mstaliti.

Kwa mujibu wa televisheni ya al Mayadeeni, kasisi Gabriel Nadaf yuko mstari wa mbele katika kuwashawishi Wakristo wa Palestina wajiunge na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linalofanya kila aina ya jinai dhidi ya Wapalestina.

Kasisi Gabriel Nadaf anatuhumiwa pia kufanya kashfa za kimaadili. Watu kadhaa waliosaidiwa na mchungaji huyo kujiunga na jeshi la Israel wamemshitaki kasisi huyo kwa jeshi la polisi la Israel kwa kuwatumia vibaya kijinsia.