HAMAS: Kuishambulia Gaza kwa mabomu, jaribio lililofeli la adui
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeashiria mashambulio ya usiku wa kuamkia leo ya jeshi katili la utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kusema kuwa, hujuma hiyo ya anga ni jaribio lililofeli la utawala wa Kizayuni la kujaribu kuonesha una nguvu.
Shirika la habari la Russia Today la Kiarabu limesisisitiza katika taarifa kuwa, utawala haramu wa Israel umetekeleza mashambulio hayo katika maeneo ya kusini na kaskazini mwa Gaza, kwa lengo la kuficha mafanio ya makundi ya muqawama katika vita vya 'Upanga wa Quuds.'
Taarifa ya HAMAS imeeleza bayana kuwa, "hujuma hizo za mabomu kamwe hazitasitisha jitihada za wanamuqawama kupigania haki zetu. Tutaendeleza mapambano haya hadi kupatikane maisha yenye uhuru na hadhi ya kibinadamu katika ardhi yetu."
Taarifa hiyo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imemalizia kwa kusema, kambi hiyo ya muqawama ipo tayari kwa machaguo yote, na katu haitauruhusu utawala ghasibu kufanikisha njama na mahesabu yake ghalati.
Duru za habari zinaarifu kuwa, ndege za kivita za utawala pandikizi wa Israel zilitekeleza mashambulio ya anga dhidi ya maeneo ya Khan Yunis, kaskazini mashariki mwa Ukanda wa Gaza jana usiku.