HAMAS: Wapalestina watapambana ili kujikomboa na kupata uhuru wao
(last modified Sun, 29 Aug 2021 14:39:28 GMT )
Aug 29, 2021 14:39 UTC
  • HAMAS: Wapalestina watapambana ili kujikomboa na kupata uhuru wao

Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS amesema, Wapalestina hawatavumilia katu kufanyiwa mapatano haki zao za kitaifa na watapambana ili kujikomboa na kupata uhuru wao.

Fawzi Barhum ameyasema hayo leo sambamba na kuashiria vitisho vilivyotolewa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel vya kuendeleza mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza na kupinga kuingizwa misaada ya kifedha na bidhaa zinazohitajika katika eneo hilo; na akasisitiza kwamba Wapalestina watatekeleza jukumu lao kuhusiana na malengo matukufu ya taifa la Palestina.

Fawzi Barhum

Kufuatia tangazo la utawala ghasibu na dhalimu wa Kizayuni la kuendeleza mzingiro dhidi ya Gaza na upinzani wake dhidi ya uingizaji misaada ya kifedha na ya bidhaa zinazohitajiwa na wakazi wa eneo hilo, makundi ya muqawama ya Palestina nayo pia yalitoa taarifa hapo jana Jumamosi na kusisitiza kuwa operesheni za ghadhabu ya usiku na urushaji maputo ya moto zitaanza tena upya.

Halikadhalika makundi ya muqawama ya Palestina yameeleza kwamba madai yanayopiganiwa na Wapalestina ni haki ya taifa hilo na yametoa onyo pia kwa utawala wa Kizayuni kuhusiana na kufanya hujuma au shambulio lolote dhidi ya wanachama wa makundi hayo ya muqawama.../

Tags