Wananchi waandamana Bahrain kumuungamkono Sheikh Ali Salman
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7945-wananchi_waandamana_bahrain_kumuungamkono_sheikh_ali_salman
Raia wa Bahrain kwa mara nyingine tena jana (Ijumaa) walifanya maandamano kuonyesha mshikamano wao kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya al Wifaq ya nchini humo, Sheikh Ali Salman.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 23:20 UTC
  • Wananchi waandamana Bahrain kumuungamkono Sheikh Ali Salman

Raia wa Bahrain kwa mara nyingine tena jana (Ijumaa) walifanya maandamano kuonyesha mshikamano wao kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya al Wifaq ya nchini humo, Sheikh Ali Salman.

Maandamano ya wananchi hao yamefanyika zikiwa zimesalia siku mbili tu hadi kutangazwa hukumu ya Sheikh Ali Salman.

Katika maandamano hayo yaliyofanywa jana baada ya swala ya Ijumaa, wananchi wa matabaka mbalimbali wa Bahrain walipiga nara dhidi ya utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa wakitaka kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa. Aidha waandamanaji wamesisitiza kukomeshwa ubaguzi kwa raia wa Bahrain. Wafanya maandamano wamelaani pia kuuliwa wanazuoni wa kidini kwa sababu za kisiasa na kutolewa hukumu nzito dhidi yao.

Rufaa ya Sheikh Ali Salman Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya nchi hiyo ilisikilizwa tarehe 12 mwezi uliopita wa Aprili nchini Bahrain, na mahakama imepanga kutoa hukumu ya mwisho tarehe 30 mwezi huu. Itakumbukwa kuwa utawala wa Aal Khalifa mwezi Juni mwaka jana ulimhukumu Sheikh Ali Salman kifungo cha miaka minne jela kwa tuhuma za kuwachochea wananchi wa Bahrain kuubadili utawala ulioko madarakani.