Kupinga Taliban kuhusu hali ya wananchi wa Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i79950-kupinga_taliban_kuhusu_hali_ya_wananchi_wa_afghanistan
Kundi la Taliban limepinga pakubwa ripoti mbalimbali zilizotolewa kuhusu hali ya mambo inayowakabili wananchi wa Afghanistan na halipo tayari kukubali uhakika wa mambo wa jamii ya nchi hiyo hasa baada ya kundi hilo kuchukua madaraka huko Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 04, 2022 02:35 UTC
  • Kupinga Taliban kuhusu hali ya wananchi wa Afghanistan

Kundi la Taliban limepinga pakubwa ripoti mbalimbali zilizotolewa kuhusu hali ya mambo inayowakabili wananchi wa Afghanistan na halipo tayari kukubali uhakika wa mambo wa jamii ya nchi hiyo hasa baada ya kundi hilo kuchukua madaraka huko Afghanistan.

Sambamba na kuanza msimu wa baridi kali, suala la ajira huko Afghanistan lingali limepungua; na wananchi wanaamini kuwa kupungua thamani ya sarafu ya nchi hiyo mkabala wa dola, kuzuiwa na Marekani akiba ya fedha za nchi hiyo, na serikali kushindwa kuwalipa walimu mishahara ni baadhi ya mambo yaliyosababisha kuanguka uchumi na kuongezeka bei na gharama za maisha huko Afghanistan.  

Ingawa maafa ya vita yamefikia ukomo baada ya kundi la wanamgambo wa Taliban kuidhibiti Afghanistan; huku utulivu wa kiwango fulani ukipatikana nchini humo lakini matatizo ya kiuchumi yangali yanawaandama wananchi wa Afghanistan kiasi kwamba wakazi wa mji mkuu Kabul pia wanakabiliwa na matizo na kushindwa hata kujidhaminia mkate wa kula. Hata kama baadhi ya ripoti za duru za Magharibi kwa mtazamo wa Taliban zinaweza kuwa zenye kukinzana lakini matamshi ya David Beasley Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) anaamini kuwa kundi la Taliban halipasi kupuuza na kuwekwa kando katika kudhoofisha na kuifanya hali ya mambo ya watu wa Afghanistan kuwa mbaya zaidi. Anaamini kuwa karibu Waafghani milioni 23 hawana chakula cha kutosha na wanakaribia kukabiliwa na baa la njaa huku wengine zaidi ya milioni 8 na laki 7 pia wakitaabika kupata chakula. Hii ina maana kuwa kama kweli Taliban inataka kuendelea kushika hatamu za uongozi huko Afghanistan basi kundi hilo halina chaguo jingine bali kukubali matakwa ya kisiasa yaani kuunda serikali shirikishi nchini humo; ambayo pia ni takwa la watu wa Afghanistan.  

Uhaba wa chakula Afghanistan 

Uongozi wa Taliban unapasa kukubali ukweli huu kwamba jamii ya leo ya Afghanistan ni tofauti sana na ile ya miongo miwili iliyopita. Taliban imefunga akthari ya ajira na hivyo kusababisha idadi kubwa ya watu kusalia bila shughuli ya kufanya wakiwemo wanawake. Pir Mohammad Mullazehi mchambuzi wa masuala ya kisiasa anazungumzia jambo hilo akisema: Taliban haina njia nyingine isipokuwa kukubali mabadiliko yaliyojitokeza katika jamii ya Afghanistan katika miongo miwili iliyopita; na hilo linaweza kupatia ufumbuzi sehemu kubwa ya matatizo waliyonayo Waafghani na jamii ya kimataifa.  

Hata kama aghalabu ya nchi jirani na wafadhili wa kimataifa wanatuma misaada ya dawa na chakula huko Afghanistan, lakini misaada hiyo tajwa ni kiwango cha chini sana kulinganisha na mahitaji ya wananchi wa nchi hiyo; huku uhaba wa bidhaa muhimu kama dawa ikiwa changamoto na daghadagha kuu ya wananchi wa Afghanistan. Kwa msingi huo, kundi la Taliban halipasi kufumbia macho matatizo na masaibu ya watu wa nchi hiyo na kutafsiri uhakika wa mambo kwa mujibu wa mtazamo wa kundi hilo. Rui Sefati mchambuzi wa masuala ya Afghanistan anaamini kuhusiana na hilo kwamba kuna hitilafu tu za mitazamo kati ya kile kilichopo huko Afghanistan na kile kinachotazamwa na Taliban. Ala kulli hal hakuna anayeweza kupuuza matatizo makubwa yanayowakabili watu wa nchi hiyo. 

Wanawake wa Afghanistan ni kati ya waliopoteza ajira nchini humo 

Kivyovyote vile, kwa kuingia madarakani, Taliban imepata fursa muhimu kwa ajili ya kuijenga upya Afghanistan bila ya kuhitaji uingiliaji wa nchi ajinabi, hata hivyo hilo halimaanishi kuhodhi siasa na kuyapuuza makundi mengine ya kikabila na kidini ya nchi hiyo, bali kwa kuasisi serikali ya umoja wa kitaifa kundi la Taliban linaweza kujiimarisha na kuthibitisha kuungwa kwake mkono na wananchi, na wakati huo huo kuhuisha nchini utawala wa kidemokrasia uliojengeka kwenye misingi ya jadi na kitaifa ya nchi hiyo.