Hamas yakaribisha juhudi za kufikia umoja wa kitaifa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i8023-hamas_yakaribisha_juhudi_za_kufikia_umoja_wa_kitaifa_palestina
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas amekaribisha juhudi zozote zenye lengo la kufanikisha umoja wa kitaifa na kuhitimisha mgawanyiko na hitilafu za ndani kati ya Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2016 02:55 UTC
  • Hamas yakaribisha juhudi za kufikia umoja wa kitaifa Palestina

Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas amekaribisha juhudi zozote zenye lengo la kufanikisha umoja wa kitaifa na kuhitimisha mgawanyiko na hitilafu za ndani kati ya Wapalestina.

Mahmoud al Zahari ameashiria uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi wa kuendesha kikao cha kimataifa kitakachoyashirikisha makundi ya Palestina kwa minajili ya kuchunguza kadhia ya mapatano ya kitaifa na kueleza kuwa, juhudi zinazofanywa na nchi yoyote katika uwanja huo ili kutekeleza makubliano yaliyosainiwa mwezi Mei mwaka 2011 mjini Cairo Misri kati ya harakati za Hamas na Fat-hو zinapasa kupongezwa.

Hata hivyo mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas amekosoa mikakati inayofanywa na harakati ya Fat-h kupitia kuendesha vikao vya kimataifa chini ya anuani "mapatano ya kitaifa" kwa shabaha ya kuiondoa Hamas katika uwanja wa siasa za Palestina na kubainisha kuwa, makombora ya muqawama yataendelea kuvurumishwa hadi pale ardhi zote za Palestina zilizoghusubiwa mwaka 1948, zitakapokombolewa.

Al Zahar amesema kuwa harakati ya Fat-h inataka kuyazunguka makubaliano ya Cairo kupitia vikao vyake vya kimataifa inavyoitisha na kwamba mapatano ya kitaifa ni istilahi inayopotoshwa.