Az-Zahar: Operesheni ya al-Khadhirah kilikuwa kibao walichozabwa wafanya mapatano
(last modified Tue, 29 Mar 2022 07:57:14 GMT )
Mar 29, 2022 07:57 UTC
  • Az-Zahar: Operesheni ya al-Khadhirah kilikuwa kibao walichozabwa wafanya mapatano

Mahmoud az-Zahar, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, operesheni ya al-Khadhirah kilikuwa kibao ambacho walichapwa wafanyamapatano na wale walio kitu kimoja na utawala ghasibu wa Kizayuni.

Usiku wa kuamkia jana, askari wawili wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel waliangamizwa na wengine 12 walijeruhiwa katika operesheni iliyotekelezwa katika mji wa al-Khadhirah kaskazini ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wapalestina wawili waliowashambulia askari hao wa Kizayuni waliuawa shahidi katika operesheni hiyo ya muqawama.

Mahmoud az-Zahar, kiongozi mwandamizi wa Hamas amebainisha kuwa, operesheni ya al-Khadhirah imeonyesha kwamba, muqawama wa Palestina ungali unaendelea.

Katika Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina Muhammad al-Ghul amesema, ujumbe wa operesheni ya al-Khadhirah ni kwamba, wananchi wa Palestina wataendeleza muqawama wao wa kupambana na uvamizi na ukaliaji kwa mabavu wa ardhi zao.

Mkutano wa usaliti wa Naqab

Al-Ghul amebainisha kuwa, mkutano wa Naqab uliohudhuriwa na baadhi ya nchi za Kiarabu utazifedhehesha na kuziaibisha tu nchi hizo na kuonyesha usaliti unaofanywa dhidi ya malengo matukufu ya Palestina.

Kikao cha pande sita cha Naqab kilifanyika siku ya Jumapili katika eneo hilo la Palestina lililovamiwa na kuanza kukaliwa kwa mabavu na wazayuni mwaka 1948, kwa kuhudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Imarati, Bahrain na Morocco na vilevile mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na wa utawala haramu wa Israel.../ 

Tags