Saudia yakiuka makubaliano ya kusimamisha vita Yemen mara 119
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82176-saudia_yakiuka_makubaliano_ya_kusimamisha_vita_yemen_mara_119
Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umekiuka makubaliano ya kusimamisha vita kwa muda wa miezi miwili huko nchini Yemen zaidi ya mara 119 ndani ya saa 24 zilizopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2022 07:25 UTC
  • Saudia yakiuka makubaliano ya kusimamisha vita Yemen mara 119

Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umekiuka makubaliano ya kusimamisha vita kwa muda wa miezi miwili huko nchini Yemen zaidi ya mara 119 ndani ya saa 24 zilizopita.

Kanali ya televisheni ya al-Masira imetangaza kuwa, muungano huo wa kijeshi wa Saudia mapema leo Jumanne umeshambulia kwa makombora mji wa Hais wa kaskazini magharibi mwa Yemen.

Ripoti hiyo ya al-Masira iliyonukuliwa na shirika la habari la Iran Press imeongeza kuwa, muungano huo vamizi umeshambulia pia kwa maroketi mkoa wa pwani wa al-Hudaidah, magharibi mwa Yemen licha ya kutangaza kuafiki mpango wa kusitisha vita kwa muda.

Kabla ya hapo, Saudi Arabia wa waitifaki wake walishambulia kwa makombora na mizinga eneo la makazi ya raia katika mkoa wa Kaskazini Magharibi wa Sa'ada nchini Yemen, na kuua raia watatu.

Aprili 2, Hans Grundberg, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen alisema kuwa, pande zinazopigana nchini humo zimekubaliana na mpango wa umoja huo wa kusimamisha vita kwa muda wa miezi miwili, kuanzia Jumamosi iliyopita.

Hujuma za Saudia kwa kutumia mabomu ya vishada Yemen

Harakati ya Ansarullah ilikuja na ubunifu huo wa kusimamisha vita na ndiyo iliyotangulia kutangaza siku tatu za kujitolea kutoshambulia maeneo ya Saudi Arabia. 

Katika hatua nyingine, taasisi ya Yemen Executive Mine Action Centre (YEMAC) imesema muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia, umedondosha mabomu ya vishada milioni 3 katika vita vya zaidi ya miaka 7 dhidi ya taifa la Yemen.