Migogoro isiyoisha Israel, serikali ya Kizayuni yachungulia kaburi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82242-migogoro_isiyoisha_israel_serikali_ya_kizayuni_yachungulia_kaburi
Muungano tawala wa utawala wa Kizayuni unaoongozwa na Naftali Bennett unachungulia kaburi hivi sasa baada Idit Silman kutoka chama cha Yamina cha Bennett mwenyewe, kutangaza ghafla kujiuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 07, 2022 06:00 UTC
  • Migogoro isiyoisha Israel, serikali ya Kizayuni yachungulia kaburi

Muungano tawala wa utawala wa Kizayuni unaoongozwa na Naftali Bennett unachungulia kaburi hivi sasa baada Idit Silman kutoka chama cha Yamina cha Bennett mwenyewe, kutangaza ghafla kujiuzulu.

Muungano huo uliundwa karibu miezi 10 illiyopita yaani tarehe 13 Juni, 2021. Unaundwa na vyama vinane na kabla ya kujitoa Idit Silman, ulikuwa na viti 61 kati ya viti 120 vya Bunge la utawala wa Kizayuni. Viti vingine 59 vilikuwa mikononi mwa vyama vya upinzani na vya Waarabu.

Kitendo cha idit Silman cha kujitoa katika muungano tawala wa Bennett kimeupokonya wingi wa kura muungano huo na sasa hivi idadi yao ni viti 60 kama ilivyo ya wapinzani. Maana ya jambo hilo ni kwamba hivi sasa serikali ya Naftali Bennet na Yair Lapit haitoweza kupasisha muswada wowote bungeni ila kwa uungaji mkono wa vyama vilivyoko nje ya muungano tawala kama mrengo wa Orodha ya Pamoja ya Waarabu.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyounda serikali tete ya Israel, Bennet ilikuwa awe waziri mkuu hadi mwezi Agosti 2023 na baada ya hapo cheo hicho cha waziri mkuu kiende kwa Yair Lapid, wa chama cha Yesh Atid hadi utakapoitishwa uchaguzi mwingine. Lakini tangu mwanzo ilitabiriwa kuwa serikali hiyo haitofika mwisho wa muda iliojipangia. Migogoro haiishi ndani ya utawala pandikizi wa Kizayuni na hivi sasa pia utawala huo unatarajiwa kuingia kwenye mkwamo na mgogoro mwingine mkubwa wa kisiasa. Serikali ya hivi sasa ya utawala wa Kizayuni iliundwa baada ya mgogoro mkubwa uliopelekea kufanyika chaguzi tano za bunge katika kipindi cha chini ya miaka miwili.

Idit Silman akizungumza kitu bungeni akiwa ameziba mdomo wake kwa mkono kukwepa vyombo vya habari

 

Swali linalojitokeza hapa ni kwamba, ni kitu gani kimepelekea serikali tete ya hivi sasa ya Israel ikumbwe na mgogoro mpya ambao unatishia kuisambaratisha?

Inavyoonekana ni kuwa,kiongozi wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu amemrubuni Idit Silman ajitoe kwenye muungano tawala na kumuahidi kumpa nafasi ya waziri wa afya ndani ya serikali mpya. Tab'an Idit Silman yeye amedai kuwa amejitoa kwenye muungano tawala kutokana na kile alichosema madhara kwa utambulisho wa Kiyahudi wa Israel. Maneno hayo yanaonesha kuwa, Silman, kama ilivyo misimamo ya Wazayuni wengi wa mrengo wa kulia, amechukizwa na kufeli mtawalia kiusalama serikali ya Kizayuni. Fursa hiyo tab'an haiwezi kuachwa vivi hivi na watu wenye hila na ubazazi wa kisiasa kama Benjamin Netanyahu. Naam, ulaghai wa kisiasa na ukatili umekita mizizi kwenye kila kona ya utawala pandikizi wa Kizayuni.

Naftali Bennett

 

Wakati serikali ya Bennett ilipojaribu kufanya mazungumzo ya Sharm al Sheikh, Aqaba na al Naqab, ilitaka kuonesha kuwa imeweza kuimarisha uhusiano wa utawala wa Kizayuni na nchi za Kiarabu bila ya hata kujitia kitanzi cha utatuzi wa kadhia ya Palestina. Lakini katika kipindi cha wiki moja tu, kumetokea opereshenei tatu dhidi ya Israel katika maeneo ya Bi'r al Sab'i, al Khadhra na Bnei Brak ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948 ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel. Wazayuni 11 wameangamizwa kwenye operesheni hizo na wengine 19 kujeruhiwa.

Pamoja na hayo kuna na uwezekano mwingine wa upande wa pili wa sarafu. Imezoeleka kuuona utawala wa Kizayuni ukizusha jambo fulani la kudanganya watu kila pale inapotaka kukwepa kutekeleza majukumu na ahadi zake. Silaha inayotumiwa na Wazayuni ni pamoja na kuzusha ombwe la utawala ndani ya Israel na kuonesha hakuna wa kutekeleza ahadi hizo kwa wakati huo. Utawala wa Kizayuni umekuwa ukitumia sana ulaghai huo wa kisiasa hasa wakati wa mazungumzo ya amani. Hila ya utawala wa Kizayuni ni kupoteza wakati na mara zote umekuwa wa kwanza kuvuruga mazungumzo kati yake ya Wapalestina. Zaidi ya hayo, wako baadhi wanasema kuwa, kwa vile hivi sasa mazungumzo ya JCPOA ya mradi wa nyuklia wa Iran yanaelekea kumalizika, Wazayuni wanataka kuishughulisha Marekani na mkwamo wa kisiasa ndani ya utawala wa Kizayuni na kuipa kisingizio serikali ya Joe Biden cha kutofikisha mwisho mazungumzo ya Vienna.