Rusia: Nato inachochea machafuko Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i826-rusia_nato_inachochea_machafuko_mashariki_ya_kati
Wizara ya Ulinzi ya Russia imejibu tuhuma za shika la kijeshi la nchi za Magharibi (NATO) ikisema muungano huo wa kijeshi imeitumbukiza Syria katika matatizo makubwa na kusababisha machafuko katika eneo lote la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 08, 2016 07:14 UTC
  • Rusia: Nato inachochea machafuko Mashariki ya Kati

Wizara ya Ulinzi ya Russia imejibu tuhuma za shika la kijeshi la nchi za Magharibi (NATO) ikisema muungano huo wa kijeshi imeitumbukiza Syria katika matatizo makubwa na kusababisha machafuko katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Meja Jenerali Igor Konashenkov amesema kuwa nchi wanachama wa NATO zimechukua hatua ambazo zimelitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati katika machafuko na vita na kwamba operesheni za kijeshi za Russia dhidi ya makundi ya kigaidi si sababu ya hali ya sasa katika eneo hilo.

Igor Konashenkov ameongeza kuwa matamshi yaliyotolewa siku chache zilizopita na Katibu Mkuu wa jumuiya ya NATO, Jens Stoltenberg ni ya kipumbavu.

Katibu Mkuu wa NATO alidai kuwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia dhidi ya makundi ya waasi nchini Syria yanadhoofisha jitihada za kupatikana njia ya utatuzi wa amani wa vita nchini Syria!