Yemen yafanya shambulio kuizuia Saudi Arabia isiibe mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89588-yemen_yafanya_shambulio_kuizuia_saudi_arabia_isiibe_mafuta
Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza shambulio la onyo dhidi ya meli ya mafuta ya Saudi Arabia iliyojaribu kuiba mafuta ghafi yanayohitajika pakubwa kutoka kwenye kituo cha mafuta kusini mwa Yemen.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Oct 23, 2022 01:05 UTC
  • Yemen yafanya shambulio kuizuia Saudi Arabia isiibe mafuta

Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimetekeleza shambulio la onyo dhidi ya meli ya mafuta ya Saudi Arabia iliyojaribu kuiba mafuta ghafi yanayohitajika pakubwa kutoka kwenye kituo cha mafuta kusini mwa Yemen.

Msemaji wa jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree  amesema kuwa jeshi la nchi hiyo lilitekekeleza shambulio hilo la kuionya Saudi Arabia baada ya meli ya nchi hiyo kujaribu kuiba mafuta katika bandari ya Dabba katika mkoa wa Hadhramaut kusini mwa Yemen. 

Yemen imetekeleza shambulio hilo katika juhudi za kuzuia hatua mtawalia za kuiba utajiri wa mafuta wa Yemen ambao ungetumika katika kulipa mishahara ya wananchi. Brigedia Jenerali Saree ameongeza kuwa,: "Vkosi vya jeshi la ulinzi vya Yemen havitasita kuzuia meli yoyote inayojaribu kuiba utajiri wa watu wa Yemen."  "Tunao uwezo wa kutekeleza oparesheni zaidi za tahadhari kwa minajili ya kuwalinda wananchi wa Yemen", ameongeza msemaji wa jeshi la Yemen.  

Utawala wa Saudi Arabia ulianzisha hujuma na uvamizi mkubwa dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka 2015 kwa kushirikiana na nchi kadhaa waitifaki wake huku ikipokea silaha na misaada ya kilojistiki kutoka kwa Marekani na nchi kadhaa za Magharibi. 

Muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia umeshindwa kutimiza malengo yake licha ya kuuwa makumi ya maelfu ya raia wa Yemen na kuitumbukiza nchi hiyo katika maafa makubwa zaidi ya kibinadamu duniani.