Mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain akamatwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9109-mkuu_wa_kituo_cha_haki_za_binadamu_bahrain_akamatwa
Katika kuendelea ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Bahrain, wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa wamemtia mbaroni Nabil Rajab, mkuu wa kituo cha haki za binadamu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2016 03:20 UTC
  • Mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain akamatwa

Katika kuendelea ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Bahrain, wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa wamemtia mbaroni Nabil Rajab, mkuu wa kituo cha haki za binadamu nchini humo.

Kwa mujibu wa Samia Rajab, mkewe Nabil Rajab, wanajeshi wa utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa walihujumu nyumba yao na kumkamata mtetezi huyo wa haki za binadamu. Nabil Rajab ametiwa mbaroni mara kadhaa tokea mwamko wa Kiislamu uanze katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi mwaka 2011.

Nabil ,ambaye pia ni mwanzilishi ya Kituo cha Haki za Binadamu cha Ghuba ya Uajemi, amekuwa mkosoaji mkubwa wa ukandamizaji na ukatili unaotumiwa na utawala wa Aal Kalifa kuzima maandamano ya amani ya wananchi.

Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya raia wa nchi hiyo tangu mwaka 2011 dhidi ya utawala ulioko madarakani wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutendewa uadilifu, kukomeshwa vitendo vya kibaguzi na kuingia madarakani serikali halali ya kidemokrasia.