HAMAS yatwaa droni ya kijasusi ya utawala haramu wa Israel
(last modified Tue, 31 Jan 2023 07:00:42 GMT )
Jan 31, 2023 07:00 UTC
  • HAMAS yatwaa droni ya kijasusi ya utawala haramu wa Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imefanikiwa kutwaa ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya utawala haramu wa Israel iliyokuwa ikiruka katika anga ya Ukanda wa Gaza.

Brigedi ya Izzudeen Qassam, tawi la kijeshi la HAMAS imesema katika taarifa kuwa, wahandisi wa harakati hiyo ya muqawama ya Palestina wamefanikuwa kupata taarifa 'hasasi' na muhimu kutoka kwenye droni hiyo aina ya hexacopter ya Wazayuni.

Utawala pandikizi wa Israel umekuwa ukikwepa kulizungumzia suala hili la kutwaliwa droni yake ya kijasusi na wanamuqawama wa Palestina. HAMAS imebainisha kuwa, droni hiyo ya kijasusi ilitwaliwa na Bridegi ya Qassam alfajiri ya Ijumaa iliyopita ikiruka katika anga ya Ukanda wa Gaza. 

Baada ya HAMAS kufichua habari ya kutwaliwa droni hiyo, utawala haramu wa Israel kupitia msemaji wake hatimaye ulikiri kuwa, 'kitu kinachofanana na droni yake' kimetua Gaza. 

Katika miezi ya hivi karibuni, ndege zisizo na rubani, ndege za kijeshi, helikopta na mizinga ya utawala wa Kizayuni imekuwa ikitumika kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza. HAMAS imefanikiwa kutungua akthari ya droni hizo za Wazayuni.

Mabaki ya droni ya Israel iliyotunguliwa na HAMAS miezi michache nyuma

Makundi ya muqawama ya Palestina yanasisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unatumia kila nyenzo ya ukatili na utumiaji mabavu kulipgisha magoti taifa la Palestina, lakini Wapalestina hawatasalimu amri katu, na wako tayari kukabiliana na Wazayuni wakati wowote na mahali popote.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS inasisitiza kuwa, jinai za kila uchao za utawala huo wa Kizayuni hazitapita hivi hivi bila kupatiwa majibu.

 

Tags