Sheikh Isa Qasim: Aal Khalifa imedhamiria kuing'oa mizizi ya Uislamu Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94062-sheikh_isa_qasim_aal_khalifa_imedhamiria_kuing'oa_mizizi_ya_uislamu_bahrain
Sheikh Isa Qasim, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ametangaza kuwa, utawala wa Aal Khalifa unafanya kila njia ili kuufuta Uislamu nchini humo.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Feb 14, 2023 23:00 UTC
  • Sheikh Isa Qasim: Aal Khalifa imedhamiria kuing'oa mizizi ya Uislamu Bahrain

Sheikh Isa Qasim, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ametangaza kuwa, utawala wa Aal Khalifa unafanya kila njia ili kuufuta Uislamu nchini humo.

Miaka 12 iliyopita katika siku kama ya jana ya tarehe 14 Februari 2011, wananchi wa Bahrain walisimama kupaza sauti zao kwa lengo la kupigania kuanzishwa mfumo wa utawala unaotokana na ridhaa ya wananchi wenyewe na kupinga dhulma, uonevu na utovu wa uadilifu wa utawala wa Aal-Khalifa.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Al-A'had ya Lebanon, Sheikh Qasiem kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kutimia miaka 12 ya vuguvugu la mapinduzi ya Bahrain la Februari 14, 2011, kwamba Februari 14 ilitokea ili kutangaza na kuhuisha tena ahadi ya kubadilisha hali ya giza totoro inayotawala Bahrain.
Sheikh Qasim ameongeza kuwa, kuna watu wenye fikra njema, wanaharakati wa kisiasa na viongozi waliofungwa jela nchini Bahrain, kama ambavyo jela hizo zina watoto wadogo ambao kosa lao pekee ni kushtushwa na sauti ya dhalimu wakaamua kuingia barabarani kulalamikia na kupinga sauti ya dhulma.
Maandamano ya vuguvugu la Februari 14 nchini Bahrain

Ayatullah Isa Qasim ameashiria njama na uungaji mkono wa hujuma dhidi ya matukufu ya Waislamu na kuzuiwa maandamano ya kulaani kuchomwa moto Qur'ani nchini Bahrain kwa kisingizio kwamba maandamano hayo ni kinyume cha sheria na akasisitiza kuwa: Uislamu hautambuliwi rasmi nchini Bahrain. Yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu si haramu nchini humo; na kwamba huko Bahrain, zinafanywa njama za kuutokomeza Uislamu; na ni kwa sababu hiyo ndio maana nchini Bahrain, inabidi usubiri ruhusa ya kisheria ya kusali Sala za jamaa na Ijumaa na kutekeleza ibada za kidini.

Akigusia suala la kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Bahrain na utawala haramu wawa Kizayuni wa Israel, Sheikh Qasim amesema, mbali ya manufaa ya kimaada ambayo Israel imepata kutokana na mahusiano hayo, lengo lake kuu na kubwa zaidi ni kuifanya jamii ya Kiislamu ya Bahrain kuwa ya Kimagharibi na kuuhamishia utamaduni wa Kiislamu kwenye utamaduni wa Magharibi.
Kwa kumalizia Sheikh Qasim amesema, nchini Bahrain zinatawala siasa na sera ya dhulma na dhalimu, sera ambayo imefeli na kugonga mwamba.../