Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu waanza mjini Baghdad
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94982-mkutano_wa_kimataifa_wa_umoja_wa_kiislamu_waanza_mjini_baghdad
Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wenye lengo la kukuribisha pamoja mitazamo ya Kiislamu na kuimarisha umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu umeanza kazi zake huko Baghdad nchini Iraq kwa juhudi za Diwani ya Waqf wa Kisuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 11, 2023 09:45 UTC
  • Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu waanza mjini Baghdad

Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wenye lengo la kukuribisha pamoja mitazamo ya Kiislamu na kuimarisha umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu umeanza kazi zake huko Baghdad nchini Iraq kwa juhudi za Diwani ya Waqf wa Kisuni.

Mkutano huo unafanyika kwa kaulimbiu "Mwislamu ni Ndugu wa Mwislamu Mwenzake."

Sheikh Khaled al-Mulla, mkuu wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, amefungua mkutano akizungumzia maana ya umoja na mshikamano wa Kiislamu. Sheikh Al-Mulla amesema kwamba, moja ya maana za umoja wa Kiislamu ni kwamba Waislamu wote wanasimama katika safu na handaki moja dhidi ya maadui wa Uislamu wanaoongozwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani ambayo inataka kupora akili, maadili, utajiri na dini ya watu.

Waziri Mkuu wa Iraqi, Mohammed Shia al-Sudani, wanafikra na wanazoni wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu kutoka nchi tofauti duniani walitazamiwa kuhutubia mkutano huo. 

Mada kuu ya Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wa Baghdad ni udharura wa kuimarishwa umoja wa Kiislamu na changamozo zinazoukabili Umma.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa, makubaliano ya hivi karibuni ya kurejesha uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia ambazo ni nchi mbili zenye ushawishi katika Ulimwengu wa Kiislamu, yanapaswa pia kugusiwa katika mada za mkutano huo.

Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu, Baghdad

Miongoni mwa mada za Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wa Baghdad ni masuala kama vile dhana ya umoja kwa mtazamo wa Kiislamu, kuishi pamoja kwa amani katika Qur'ani na Suna, suala la utakfiri katika fiqhi ya Kiislamu, kanuni za hitilafu za kifikra katika Sharia na maadili, njia za kukabiliana na mpango wa kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel, jukumu la vyombo vya habari katika kuimarisha umoja na vilevile dini na athari zake katika kuishi pamoja kwa amani.