Mataifa ya Ulaya yakosoa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i95160-mataifa_ya_ulaya_yakosoa_ujenzi_wa_vitongoji_vya_walowezi_wa_kizayuni
Mataifa kadhaa ya Ulaya yamekosoa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel huko Palestina na kutoa mwito wa kukomeshwa mara moja sera hizo ambazo ni kinyume cha sheria za kimataifa.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Mar 16, 2023 04:10 UTC
  • Mataifa ya Ulaya yakosoa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

Mataifa kadhaa ya Ulaya yamekosoa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel huko Palestina na kutoa mwito wa kukomeshwa mara moja sera hizo ambazo ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Mataifa 17 ya Ulaya ambayo mengi kati ya hayo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya sambamba na kukosoa sera za utawala ghasibu wa Israel yametaka kuhitimishwa sera za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kufukuzwa familia za Kipalestina kutoka katika nyumba zao mashariki mwa Baytul-Muqaddas.

Taarifa ya mataifa hayo ya Ulaya ambayo yanajumuisha Uingereza, Ufaransa, Uhispania na Uholanzi imebainisha upinzani wake mkali dhidi ya ujenzii wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza: Inatia wasiwasi mno kusikia kwamba, viongozi wa Israel wana mpango wa kuendeleza siasa zao za uharibifu na kubomoa nyumba za Wapalestina katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Israel imekuwa ikibomoa nyumba za Wapalestina na badala yake kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

 

Mwezi uliopita wa Februari, kundi la nchi za Amerika ya Latini lililaani na kukosoa vikali uamuzi wa serikali ya Israel yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya tisa katika ardhi za Wapalestina za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Tarehe 20 ya mwezi uliopita wa Februari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha rasimu ya azimio linalolaani uamuzi wa serikali ya Israel yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya tisa katika ardhi za Wapalestina za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.