Miaka 8 ya vita Yemen; Muqawama wazidi kuimarika na kushikamana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i95568-miaka_8_ya_vita_yemen_muqawama_wazidi_kuimarika_na_kushikamana
Wananchi wa Yemen jana walifanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a na katika miji mingine ya nchi hiyo kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa nane wa mapambano ya wananchi wa Yemen mkabala wa vita na mzingiro uliowekwa dhidi ya nchi hiyo na muungano vamizi wa Saudia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2023 04:14 UTC
  • Miaka 8 ya vita Yemen; Muqawama wazidi kuimarika na kushikamana

Wananchi wa Yemen jana walifanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a na katika miji mingine ya nchi hiyo kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa nane wa mapambano ya wananchi wa Yemen mkabala wa vita na mzingiro uliowekwa dhidi ya nchi hiyo na muungano vamizi wa Saudia.

Tarehe 26 Machi 2015 ni siku ya kukumbuka kuanza kwa uvamizi wa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia. Kwa mnasaba huo, makundi mbalimbali ya Wayemen jana yalifanya maandamano makubwa katika mji mkuu Sana'a na katika miji mingine ya nchi hiyo. 

Ripota wa Iran Press huko Sana' a amefanya mahojiano na viongozi na wanaharakati kadhaa wa kisiasa wa nchi hiyo katika kuwadia mwaka wa nane wa mapambano ya wananchi wa Yemen dhidi ya uvamizi wa muungano wa Saudia.  

Ahmad Hamed Mkuu wa Ofisi ya  Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema pambizoni mwa maandamano hayo kuwa: nguvu, mshikamano na uthabiti wa watu wa Yemen umeongezeka katika kipindi cha miaka minane ya vita vya wavamizi dhidi yao.