Ujumbe wa Oman wawasili Sana'a kufanikisha mapatano mapya ya kusitisha vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i96066-ujumbe_wa_oman_wawasili_sana'a_kufanikisha_mapatano_mapya_ya_kusitisha_vita
Ujumbe wa Oman umewasili Sana'a mji mkuu wa Yemen katika jitihada za kufanikisha mapatano mapya ya usitishaji vita kati ya harakati ya Ansarullah na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia. Muungano huo umekuwa ukiendesha vita huko Yemen tangu mwaka 2015.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2023 04:52 UTC
  • Ujumbe wa Oman wawasili Sana'a kufanikisha mapatano mapya ya kusitisha vita

Ujumbe wa Oman umewasili Sana'a mji mkuu wa Yemen katika jitihada za kufanikisha mapatano mapya ya usitishaji vita kati ya harakati ya Ansarullah na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia. Muungano huo umekuwa ukiendesha vita huko Yemen tangu mwaka 2015.

Ujumbe huo wa Oman uliwasili jana Sana'a kujadili hatua zilizopigwa katika mazungumzo yanayoendelea huko Muscat. Ujumbe huo uliwasili Yemen ili  kufanya pia mazungumzo na viongozi wa harakati ya Ansarullah kuhusu mapatano ya kusitisha vita na mchakato wa amani. 

Saudi Arabia na nchi kadhaa waitifaki wake zilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka 2015 baada ya harakati ya Ansarullah kudhibiti masuala ya Yemen.  

Vita vya Yemen hadi sasa vimeuwa mamia ya maelfu ya Wayemeni na kuigeuza nchi nchi hiyo kuwa eneo ambalo Umoja wa Mataifa umelitaja kuwa lililoathiriwa pakubwa na maafa ya binadamu duniani licha ya  muungano vamizi wa Saudia kushindwa kutimiza malengo yake huko Yemen.