Al Houthi: Hatua za kivitendo za Riyadh zitafanikisha mazungumzo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i96528-al_houthi_hatua_za_kivitendo_za_riyadh_zitafanikisha_mazungumzo
Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa kupiga hatua kivyovyote katika mchakato wa mazungumzo kati yao na muungano vamizi wa Saudia kutategemea na hatua za kivitendo za Riyadh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 21, 2023 22:10 UTC
  • Al Houthi: Hatua za kivitendo za Riyadh zitafanikisha mazungumzo

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa kupiga hatua kivyovyote katika mchakato wa mazungumzo kati yao na muungano vamizi wa Saudia kutategemea na hatua za kivitendo za Riyadh.

Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Saudia na Yemen ilifanyika wiki jana kufuatia ziara iliyofanywa huko Sanaa na Mohammed bin Saeed Al-Jaber Balozi wa Saudi Arabia huko Yemen; ambapo pande mbili zimekubaliana kuwaachia huru mateka wa vita wa pande mbili wapatao 900 ili kuonyesha nia yao njema.  

Mabadilisho ya mateka wa kivita kati ya Yemen na Saudia 

Duru ya pili ya mazungumzo ya kubadilishana mateka hao tajwa kati ya Riyadh na Sana'a imepangwa kuanza tena baada ya Sikukuu ya Idul-Fitr. Muhammad Ali al Houthi Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen alisema jana kwamba: muungano wa Saudia unapasa kusogeza mbele mazungumzo kwa kudhihirisha hatua za kivitendo.  

Al Houthi ameongeza kuwa, kipaumbele cha wananchi wa Yemen katika mazungumzo hayo na Saudia ni kukidhiwa mahitaji ya kibinadamu na kwamba,  serikali ya Sana'a haitilii umuhimu wowote mazungumzo na mashauriano ambayo hayaambatani na hatua za kivitendo za Saudi Arabia katika mazungumzo hayo.