Hamas: Sera za mauaji ya kigaidi za utawala wa Kizayuni zimeshindwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i96596-hamas_sera_za_mauaji_ya_kigaidi_za_utawala_wa_kizayuni_zimeshindwa
Baada ya kuchapishwa habari kuhusu ombi la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel la kutaka kumuua naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, msemaji wa harakati hiyo amesema vitisho hivyo na sera za ugaidi za utawala huo ghasibu zimeshindwa na kufeli.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 23, 2023 22:02 UTC
  • Hamas: Sera za mauaji ya kigaidi za utawala wa Kizayuni zimeshindwa

Baada ya kuchapishwa habari kuhusu ombi la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel la kutaka kumuua naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, msemaji wa harakati hiyo amesema vitisho hivyo na sera za ugaidi za utawala huo ghasibu zimeshindwa na kufeli.

Baada ya kushindwa jeshi la utawala wa Kizayuni katika medani za vita katika siku za hivi karibuni, maafisa kadhaa wa zamani wa utawala huo wametoa wito wa kuuawa naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, Saleh al-Aroori, kama "mwanastratijia mkuu" wa harakati hiyo.

Majenerali kadhaa na maafisa wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuomba Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, amuue Saleh al-Arouri, naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Hazem Qassem, msemaji wa Hamas amesisitiza kwamba, vitisho vya adui Mzayuni vya kutaka kuanza tena sera za mauaji ya kigaidi dhidi ya viongozi wa Hamas ni jaribio lisiloshindwa la kutaka kuboresha sura ya utawala huo baada ya kushadidi harakati za mapinduzi za wananchi wa Palestina na kupanuka kambi ya mapambano ya ukombozi.

Raia wa Palestina wakipambana na wanajeshi wa Israel, Ukingo wa Magharibi

Qassem ameongeza kuwa, mkono wa adui hauko wazi kutekeleza hujuma za kigaidi na majibu ya muqawama dhidi ya upumbavu wowote yatakuwa makubwa na mapana zaidi kuliko utawala huo unavyofikiri.

Hazem Qassem amesema, Hamas itaendelea kupambana na utawala ghasibu wa Israel na kamwe haiogopi vitisho hivyo.