Utawala wa Kizayuni wamuua shahidi Mpalestina, waharibu nyumba
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9667-utawala_wa_kizayuni_wamuua_shahidi_mpalestina_waharibu_nyumba
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamempiga risasi na kumuua shahidi kijana Mpalestina kwa kosa la kurushia gari lao jiwe na baada ya hapo kuharibu nyumba ya Mpalestina mwingine katika Ukingo wa Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2016 03:29 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wamuua shahidi Mpalestina, waharibu nyumba

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamempiga risasi na kumuua shahidi kijana Mpalestina kwa kosa la kurushia gari lao jiwe na baada ya hapo kuharibu nyumba ya Mpalestina mwingine katika Ukingo wa Magharibi.

Duru zinaarifu kuwa wanajeshi wa Kizayuni walimpiga risasi na kumuua shahidi Mahmoud Badran aliyekuwa na miaka 20 kwa tuhuma kuwa alirushia gari lao jiwa katika eneo baina ya vijiji vya Beit Sira na Beit Ur katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wapalestina wengine wawili walijeruhiwa kwa tuhuma hiyo hiyo ya kurusha mawe.

Leo Jumanne pia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamebomoa nyumba ya Mpalestina Bashar Massala kwa madai kuwa amewashambulia Wazayuni katika eneo la kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiwaua kiholela Wapalestina na kubomoa nyumba za Wapalestina kwa madai kuwa wanawashambulia Wazayuni.