Balozi Zawawi: Muda wa kukombolewa taifa la Palestina umewadia
Balozi wa Palestina nchini Iran amesema kuwa, umewadia wakati sasa kwa taifa la Palestina kukombolewa na sote tuswali katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.
Bi Salam Zawawi amesisitiza kwamba, sisi kama Wapalestina siku zote tunasema kuwa, sikukuu yetu ni sku ambayo tunaterejea katikak nchi yetu na bila ya kurejea katika ardhi za mababu zote huko Palestina hatuwezi kuwa na sikukuu.
Balozi wa Palestina mjini Tehran ameongeza kuwa, tunafanya juhudo na kkwa kutumia kila wenzo ili kuhakikisha kwamba, taifa letu la Palestina linakombolewa na kuondoka katika makucha ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Bi Salam Zawawi ameongeza kuwa, licha ya kuwa Palestina haina mamlaka kamili, lakini pamoja na hayo ina wawakilishi wa kidiplomasia katika mataifa zaidi ya 52 duniani.
Balozi wa Palestina mjini Tehran ametoa wito wa kuungwa mkono taifa madhulumu la Palestina ili liweze kupatiwa haki zake za kimsingi zilizoghusubiwa na utawala ghasibu wa Israel.
Kadhalika balozi Zawawi ameashiria matukio ya hivi karibuni huko Palestina inayyokaliwa kwa mabavu na umoja ulioko baina ya aghalabu ya makundi ya muqawama wa Palestina na kueleza kwamba, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu hivi sasa taifa madhulumu la Palestina na makundi yote ya Palestina licha ya hitilafu yalizonazo lakini yana mtazamo mmoja, nao ni kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.
Amesisitiza kuwa, huu ni ukweli ambao ni katika misingi ya fikra za Palestina na hakuna serikali au shakhsia au kundi lolote ambalo linaweza kufumbia macho jambo hili, na Inshallah kwa uwezo wa Allah, Palestina itafanikiwa katika lengo lake hili.