Mfalme wa Jordan asisitiza kuundwa taifa huru la Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i99214-mfalme_wa_jordan_asisitiza_kuundwa_taifa_huru_la_palestina
Mfalme Abdullah II wa Jordan amesisitizia suala la kuundwa taifa huru la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2023 04:25 UTC
  • Mfalme wa Jordan asisitiza kuundwa taifa huru la Palestina

Mfalme Abdullah II wa Jordan amesisitizia suala la kuundwa taifa huru la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.

Akihutubia hapo jana, Mfalme wa Jordan ameutaka utawala ghasibu wa Israel kujiepusha na vitendo ambavyo vinapelekea kuondoka fursa ya kupatikana amani ya kweli huko Palestina.

Kadhalika Mfalme huyo wa Jordan amesema kuwa, kuna haja ya kuongezwa juhudi maradufuu kwa minajili ya kupunguza mizozo na mivutano katika ardhi za Palestina.

Jordan imekuwa ikitoa mwito mara kwa mara wa kutaka kupatikana amani ya kweli na kiuadilifu itakayodhamini kuundwa nchi huru ya Palestina.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia vibaya mghafala wa jamii ya kimataifa na unazidi kufanya jinai kama kuwafukuza Wapalestina kwenye maeneo yao na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Pia unachimba mashimo katika eneo la al-Buraq lenye misikiti ya Waislamu ikiwa ni kuendeleza mradi wa Wazayuni wa kujenga hekalu la Solomon.

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno.

Madola ya Magharibi yamekuwa yakikosolewa kutokana na himaya na uungaji mkono wake kwa utawala ghasibu wa Israel na hata wengi wanaamini kuwa, himaya hiyo ndiyo inayoupa kiburi utawala huo ghasibu cha kuuendeleza hujuma na jinai zake dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.