Algeria yatenga dola milioni 30 za ujenzi mpya wa Jenin
Serikali ya Algeria imeahidi kutoa dola milioni 30 za Kimarekani kusaidia ujenzi mpya wa kambi na mji wa Jenin ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya eneo hilo kushuhudia jinnai kubwa ya utawala wa Kizayuni.
Ikulu ya Rais wa Algeria imetoa taarifa hiyo na kusisiza kuwa uamuzi huo umechukuliwa na Algiers baada ya jinai kubwa ya kijeshi iliyofanyw ana jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi wa Jenin na kambi yake ya wakimbizi. Jinai hiyo kubwa ya Wazayuni ilifanyika tangu Jumatatu hadi Jumanne.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Algeria ina nia ya kweli ya kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya wakazi wa Palestina na kuunga mkono jitihada za kuliletea taifa hilo madhlumu, mustakabali wa uhuru na ustawi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mchango huo wa kifedha unaonesha jinsi Algeria inavyoumizwa sana na kadhia ya Palestina na imeamua kujitolea kwa dhati katika kupunguza mateso wanayofanyiwa Wapalestina na utawala katili wa Israel.
Siku chache zillizopita pia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilitoa mwito wa kuadhibiwa Wazayuni wote waliohusika kwenye jinai ya Jenin.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria kwamba hujuma za Wazayuni huko Jenin ni ukiukaji wa wazi wa sheria zote za kimataifa na ni uvunjaji wa haki za kimsingi kabisa za binadamu.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Quds Al Arabi, katika taarifa hiyo, jamii ya kimataifa hususan Baraza la Usalama limetakiwa kutekeleza wajibu wake wa kisiasa na kisheria wa kuhakikisha kuwa linavutia uungaji mkono wa kimataifa kwa taifa la Palestina na kuwaadhibu Wazayuni waliofanya jinai hizo ni jambo la lazima.