-
Yemen yaonya kuhusu kushtadi jinai za Israel Gaza, Ukingo wa Magharibi
Dec 15, 2025 10:59Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imetahadharisha dhidi ya kuongezeka kwa ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, ikiukosoa utawala huo pandikizi kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kuzidisha mashambulizi.
-
WHO: Zaidi ya Wapalestina 1,000 wamefariki Gaza baada ya Israel kuwazuia kusafiri kupata matibabu
Dec 15, 2025 02:17Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema zaidi ya Wapalestina 1,000 wamepoteza maisha katika Ukanda wa Gaza kati ya Julai 2024 na Novemba 2025, wakisubiri ruhusa ya utawala wa Israel kuhamishwa kwa ajili ya matibabu kutoka kwa mamlaka za Kizayuni.
-
Hamas yalaani mauaji ya kamanda wake, raia Gaza
Dec 14, 2025 09:13Kiongozi wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, Khalil al-Hayya, katika taarifa yake ya video leo Jumapili amethibitisha kuwa, kamanda mwandamizi wa harakati hiyo, Raed Saed ni miongoni mwa watu watano waliouawa shahidi katika shambulio la Israel huko Gaza.
-
UNICEF yaonya kuhusu mlipuko wa magonjwa miongoni mwa watoto Gaza
Dec 14, 2025 07:11Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeonya juu ya ongezeko la hatari ya milipuko ya magonjwa miongoni mwa watoto katika Ukanda wa Gaza, huko Palestina.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Marekani itambue kwamba katu hatutaweka chini silaha zetu
Dec 14, 2025 02:08Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, serikali ina wajibu wa kufanya juhudi za kuzatiti mamlaka ya kujitawala na uhuru wa Lebanon, na Muqawamwa kwa upande wake umeisaidia kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Albanese: Israel na waungaji mkono wake wakuu inawapasa wagharamie ujenzi mpya wa Ghaza
Dec 13, 2025 11:36Francesca Albanese, Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesema, Israel na Marekani pamoja na nchi zingine ambazo zilikuwa wasambazaji wakuu wa silaha kwa utawala huo, zinapaswa kugharimia ujenzi mpya wa eneo la Ukanda wa Ghaza.
-
Wapalestina 14, wakiwemo watoto, wafariki dunia Gaza kutokana na baridi kali
Dec 13, 2025 06:58Wapalestina wasiopungua 14 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika kipindi cha chini ya saa 24 huku baridi na dhoruba kali ikiendelea kunguruma katika Ukanda wa Gaza, na kuangusha majengo na miundo mbinu katika maeneo kadhaa.
-
Israel yakiri: Tulisababisha uharibifu mdogo kwa Iran kuliko ilivyodhaniwa hapo awali
Dec 13, 2025 02:33Israel imekiri kuwa ilisababisha uharibifu wa kiwango kidogo kwa Iran wakati wa vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka huu kuliko ilivyofikiriwa awali.
-
Ripoti: US inaishinikiza Israel iuondoe mlima wa kifusi uliozagaa Ghaza baada ya miaka 2 ya vita
Dec 12, 2025 10:10Marekani imeitaka Israel ibebe jukumu la kuondoa vifusi vikubwa vilivyotapakaa kwenye kila pembe ya Ukanda wa Ghaza baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vya kinyama na mauaji ya kimbari iliyofanya dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo, pamoja na uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi yake ya anga na matingatinga ya kivita. Hayo yameelezwa na toleo la Alkhamisi la gazeti la kizayuni la Yedioth Ahronoth.
-
Umoja wa Mataifa: Hali ya kibinadamu Gaza ni mbaya
Dec 12, 2025 02:40Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuongezeka kwa janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mvua na baridi kali huko Palestina.