-
Nchi 14 za Kiarabu zinapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel
Jan 07, 2023 03:52Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa katika nchi 14 za Kiarabu yanaonesha kuwa, akthari ya watu wa nchi hizo wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Mwanazuoni wa Bahrain: Ni haramu kuwauzia ardhi Mayahudi
Jan 07, 2023 03:40Imamu Sala ya Ijumaa katika mji wa Al-Diraz nchini Bahrain, amesema kuwauzia ardhi Wayahudi ni sawa na kuiuza nchi na ni haramu.
-
Wayemen waandamana kitaifa dhidi ya muungano vamizi wa Saudia-Marekani
Jan 06, 2023 23:09Jana Ijumaa, wananchi wa Yemen walifanya maandamano makubwa katika mikoa mbalimbali kulaani uvamizi wa muungano wa Saudia na Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu na kuendelea kuzingirwa kila upande nchi yao pamoja na vitendo mbalimbali vya kuchochea vita vinavyofanya na madola vamizi.
-
Wasiwasi wa kieneo na kimataifa kuhusu tabia ya ubaguzi wa rangi ya baraza jipya la mawaziri la Israel dhidi ya Wapalestina
Jan 06, 2023 23:07Hatua ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa utawala haramu wa Israel, ya kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa imekabiliwa na radiamali kali ya kieneo na kimataifa, na ambayo imezipelekea nchi za China na Imarati kuomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadiliwa suala hilo.
-
Marekani ilikiuka mamlaka ya kujitawala Iraq kwa kuwaua Jenerali Soleimani na Al Muhandis
Jan 06, 2023 06:25Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani amemuenzi kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad miaka mitatu iliyopita, na kusema kuwa mauaji hayo yalikuwa "shambulio kali" dhidi ya uhuru na mamlaka ya kujitawala Iraq.
-
Kuongezeka umaarufu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani duniani, hasa barani Asia
Jan 06, 2023 04:20Sambamba na kuadhimishwa mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes, habari na ripoti zilizochapishwa kuhusu kufanyika sherehe katika maeneo mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa uungwaji mkono na umaarufu wa jenerali huyo mashuhuri umeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na hasa miongoni mwa vijana.
-
Mpalestina aliyeshikiliwa kwenye gereza la Israel kwa muda mrefu zaidi wa miaka 40 aachiwa huru
Jan 05, 2023 22:52Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umemwachilia huru mateka Mpalestina aliyeshikiliwa kwenye gereza la utawala huo dhalimu kwa muda mrefu zaidi wa miaka 40.
-
Wanaharakati wanawake 35 wa Saudia wahukumiwa kifungo cha miaka 11 jela
Jan 05, 2023 22:52Vyanzo vya mashirika ya kutetea haki za binadamu vimeripoti kuwa wanaharakati wanawake 35 wa Saudi Arabia wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela na utawala wa Al-Saud.
-
Sisitizo la kulaaniwa kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa
Jan 05, 2023 06:44Nchi za Kiarabu na Kiislamu zimesisitiza ulazima wa kulaaniwa kitendo cha Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala ghasibu wa Israel cha kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Umoja wa Ulaya washindwa kulaani uchochezi wa waziri mwenye itikadi za kibaguzi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa.
Jan 05, 2023 04:29Kitendo cha uchochezi cha waziri mwenye itikadi kali na za kibaguzi wa baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel katika kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa hakijakabiliwa na hatua yoyote ya maana kutoka kwa Umoja wa Ulaya.