-
Kuongezeka watoto wa Kipalestina katika magereza ya Israel
Nov 22, 2022 07:09Wizara ya Mateka na Wafungwa wa Kipalestina Walioachiliwa Huru kutoka gerezani imetangaza kuwa, hivi sasa kuna watoto 170 wa Kipalestina katika magereza ya Israel huku watano kati yao wakishikiliwa pasi na kuelezwa tuhuma na makosa yao.
-
Yemen yazima jaribio la meli ajinabi kuiba mafuta yake
Nov 22, 2022 03:47Vikosi vya jeshi la Yemen vimetangaza habari ya kufanikiwa kuzima jaribio la wizi wa mafuta ya nchi hiyo, lililofanywa na meli ya kubeba mafuta ya nchi ya kigeni.
-
Bin Salman na Bin Zayed hawana ubavu isipokuwa wa kuua watoto wa Kiyemen
Nov 21, 2022 22:53Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo faili la jinai za kivita la Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Sheikh Muhammad bin Zayed Al-Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko nchini Yemen linavyozidi kuwa kubwa.
-
Kombe la Dunia; Vijana wa Kiarabu wakataa kuzungumza na wanahabari wa Israel
Nov 21, 2022 07:55Mashabiki wa soka wa nchi za Kiarabu wamekataa kuzungumza na waandishi wa habari wa mashirika ya utawala haramu wa Israel nchini Qatar, kunakofanyika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu 2022; kuonyesha upinzani wao wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Nov 21, 2022 07:23Sambamba na kuanza uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita nchini Afghanistan unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito wa kuchunguzwa mashambulio ya mauaji ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
-
Idadi ya watoto waliouawa vitani nchini Yemen yapindukia 8,000
Nov 21, 2022 03:06Taasisi moja ya masuala ya sheria imetangaza kuwa, idadi ya watoto waliofanywa wahanga wa vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen imeshapindukia elfu 8.
-
UN yaalani mashambulizi ya kinyama ya walowezi na wanajeshi wa Kizayuni huko al Khalil
Nov 20, 2022 23:04Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya kinyama ya walowezi wa Kizayuni wakishirikiana na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel huko katika mji wa al Khalil.
-
Abdulsalam: Baadhi ya makundi ya Wayemen yanafaidika na kuendelea umwagaji damu
Nov 20, 2022 23:00Mkuu wa ujumbe wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo ameeleza kuwa, baadhi ya mirengo ya ndani huko Yemen yenye mfungamano na Riyadh yamegeuka na kuwa wafaidikaji katika vita huko Yemen.
-
Hamas: Mpango wa wavamizi wa Kizayuni huko al Khalil utashindwa
Nov 20, 2022 08:15Sambamba na kupongeza muqawama na mapambano ya wananchi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, msemaji wa harakati ya Hamas amesisitiza kuwa, juhudi za utawala wa Kizayuni za kuimarisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi huko al Khalil hazitafanikiwa.
-
Kuongezeka maradufu watu wanaokatwa vichwa nchini Saudi Arabia
Nov 20, 2022 05:18Serikali ya Saudia inatumia vibaya kimya cha madola makubwa na jamii ya kimataifa, kuzidisha kukata vichwa watu kwa visingizio tofauti kiasi kwamba, idadi ya watu waliotekelezewa adhabu ya kifo na ukoo wa Aal Saud mwaka huu, tayari hivi sasa ni maradufu ya waliokatwa vichwa mwaka jana nchini humo.