-
Mwisho wa satwa ya Marekani: Asia Magharibi Katika Ukingo wa Mfumo Mpya
Aug 23, 2026 06:27Katika uchambuzi wake wa hivi karibuni, jarida la Foreign Affairs linataja vita dhidi ya Iran kama hatua muhimu inayoharakisha kuporomoka kwa mfumo wa kikanda unaoongozwa na Marekani na kudhihiri taratibu mabadiliko yanayoweza kubadili mitazamo na mikakati ya kiusalama ya mataifa ya Asia Magharibi katika miaka ijayo.
-
Vitisho Visivyo na Uzito vya Trump na Kudhoofika kwa Nguvu ya Marekani
Aug 23, 2026 04:57Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena ametishia kuishambulia Oman kwa mabomu, nchi iliyo na nafasi muhimu katika mazungumzo yanayohusu Iran pamoja na masuala yanayohusiana na usafiri wa baharini katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Maafisa wa jeshi la Israel: Netanyahu anataka kushadidisha vita ili uchaguzi usifanyike
Aug 23, 2026 03:12Maafisa waandamizi wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel wanamshuku waziri mkuu Benjamin Netanyahu kwamba anaweza akataka kushadidisha vita katika Ukanda wa Ghaza ili kujaribu kuvuruga au kuahirisha uchaguzi ujao wa bunge wa utawala huo ghasibu.
-
Hizbullah: Rekodi ya serikali ya Marekani imejaa umwagaji damu na jinai
Aug 22, 2026 12:19Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali vikwazo vipya vya Wizara ya Hazina ya Marekani dhidi ya harakati hiyo.
-
Umoja wa Mataifa: Hali ya kibinadamu Ukanda wa Gaza ni mbaya kutokana na kuongezeka wimbi la njaa
Aug 22, 2026 02:53Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Israel pamoja na kushadidishwa mzingiro dhidi ya eneo hilo.
-
Miaka 57 tangu kuchomwa moto Msikiti wa Al-Aqswa; uhalifu unaoendelea kujirudia
Aug 22, 2026 02:51Miaka 57 baada ya kuchomwa moto kwa Msikiti wa Al-Aqsa, utambulisho wake wa Kiislamu unaendelea kutishiwa na njama za kuliyahudisha eneo hilo takatifu zingali zinaendeea.
-
Wapalestina ‘wanakabiliwa na baa la njaa’ huku walowezi wa Kizayuni wakiendeleza mzingiro katika mji wa Qusra
Aug 21, 2026 10:19Wapalestina walionaswa ndani ya nyumba zao katika mji wa Qusra wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku walowezi wenye itikadi kali za Kizayuni wakiendeleza mzingiro wao dhidi ya mji huo wa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, wakati vikosi vya utawala ghasibu wa Israel vikiendelea kuzuia misaada ya chakula kufika.
-
Mazishi ya Wapalestina 50 wasiojulikana waliouawa katika mauaji ya kimbari
Aug 21, 2026 06:08Mamia ya watu wameswali Swala ya Janaza wakati wa mazishi ya pamoja katika Jiji la Gaza kwa ajili ya Wapalestina 50 ambao miili yao ilipatikana hivi karibuni na vikosi vya Ulinzi wa Raia ikiwa chini ya mabaki ya nyumba zilizobomolewa katika mashambulizi ya Israel wakati wa vita vya mauaji ya kimbari katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Baada ya kukana kwa zaidi ya miaka 2, Israel yakiri kumuua mtoto wa Kipalestina Hind Rajab
Aug 20, 2026 11:40Kwa mara ya kwanza, jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limekiri kuwa lilimuua Hind Rajab mtoto wa Kipalestina mwenye umri wa miaka mitano huko Ghaza, na hivyo kubatilisha makanusho yake ya hapo awali, na kutangaza kwamba limeshaagiza kufanyika uchunguzi wa kijinai kuhusiana na mauaji yake.
-
Israel imepora hekta 25,000 za ardhi ya Ukingo wa Magharibi katika miaka mitatu iliyopita
Aug 20, 2026 03:18Utawala dhalimu wa Israel umepora hekta 25,000 za ardhi ya Ukingo wa Magharibi katika miaka mitatu iliyopita.