-
Serikal ya Lebanon hatimaye yachukua hatua za kupambana na Israel
Nov 03, 2025 03:02Baada ya kupita miezi kadhaa ya kutochukua hatua, hatimaye serikali ya Lebanon imeamua kupambana na Israel kwa kupeleka jeshi lake mpakani ili kukabiliana na uchokozi wa mara kwa mara wa utawala wa Kizayuni kwenye mipaka yake ya kusini.
-
Hamas: Tumeshikamana na ahadi za kurejesha miili ya mateka wa Kizayuni
Nov 02, 2025 22:54Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa na kutangaza kwamba, bado inaheshimu na kushikamana na ahadi zake za kukabidhi kwa Israel miili ya mateka wa Kizayuni waliouliwa na utawala wa Kizayuni wakati wa mashambulizi yake ya miaka miwili kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
Israel yaendelea kuwatesa kwa njaa Wapalestina kwa kuruhusu 24% tu ya misaada kuingizwa Ghaza
Nov 02, 2025 03:20Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimetangaza kuwa utawala wa kizayuni wa Israel umeruhusu kuingizwa katika eneo hilo sehemu ndogo tu ya misaada ya kibinadamu kinyume na ilivyoafikiwa katika makubaliano ya usitishaji mapigano yanayosimamiwa na serikali ya Marekani, ambayo yalianza kutekelezwa mwezi uliopita.
-
Israel yaendelea kukiuka makubaliano na Lebanon, yashambulia na kuua watu 4 na kujeruhi 3
Nov 02, 2025 02:57Shambulio la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limesababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine watatu kusini mwa Lebanon ukiwa ni mwendelezo wa mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na Tel Aviv ndani ya ardhi ya nchi hiyo, ambayo yanakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwishoni mwa Novemba 2024 kati ya Harakati ya Muqawama ya Hizbullah na utawala huo ghasibu.
-
UN: Gaza ni eneo hatari zaidi kwa waandishi wa habari duniani
Nov 01, 2025 23:45Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameangazia hatari zinazowakumba waandishi wa habari duniani kote, akielekeza macho hasa kwa Ukanda wa Gaza, ambapo ametaja eneo hilo la Palestina lililozingirwa na utawala wa Israel kuwa eneo hatari zaidi kwa waandishi wa habari hivi sasa dunaini.
-
Israel yakiuka usitishaji vita, yaua Wapalestina 10 kila siku
Nov 01, 2025 04:27Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Euro-Mediterania lilitangaza siku ya Ijumaa katika ripoti yake kuwa, utawala wa Kizayuni umekuwa ukiwaua shahidi Wapalestina 10 kila siku tangu kuanza kwa usitishaji vita.
-
Naeem Qassem: Muqawama ni nembo ya nguvu ya Lebanon, unapaswa kulindwa
Nov 01, 2025 03:53Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani inadai kwamba inataka kutatua matatizo ya Lebanon lakini nchi hiyo sio mpatanishi mwadilifu asiyependelea upande wowote na ni mshirika katika uhalifu na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Idara ya Habari Palestina: Kuna mabomu 20,000 ambayo hayajalipuka huko Gaza
Nov 01, 2025 03:06Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Palestina imetangaza kwamba mabomu 20,000 ambayo hayajalipuka bado yamebaki katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Erdogan amkosoa vikali Kansela wa Ujerumani: Huoni mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza?
Oct 31, 2025 23:04Rais wa Uturuki amekosoa vikali msimamo wa Ujerumani wa kuuunga mkono utawala wa Israel, akimwambia kansela wa nchi hiyo: "Je, huoni mauaji ya halaiki na njaa ya kutengeneza kwa makusudi inayowakabili watu wa Gaza?"
-
Majibu ya Ansarullah kwa Israel Katz: "Hatutamruhusu mtenda jinai atutishie"
Oct 31, 2025 07:36Mohammad al-Farah, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amejibu matamshi ya Waziri wa Vita wa Israel kwamba utawala huo ghasibu bado haujafikia malengo yake yoyote hadi sasa.