Dec 27, 2023 14:27
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kislamu mapema leo amehutubia maelfu ya wanawake na wasichana ambako amebainisha mtazamo wa kimantriki wa Uislamu kuhusu nafasi ya wanawake katika familia na shughuli kijamii, siasa na uongozi katika ngazi mbalimbali na kusisitiza kuwa: Katika Uislamu, njia ya shughuli zozote za kijamii ziko wazi kwa wanawake, sawa na ilivyo kwa wanaume, kwa sharti kwamba mambo mawili muhimu yazingatiwe, yaani suala la familia na kuchunga hatari ya mvuto wa kijinsia.