Nov 04, 2023 03:02 UTC
  • Balozi wa Cuba: Israel ndiye gaidi halisi

Balozi wa Cuba mjini Tehran sanjari na kulaani jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, ameutaja utawala huo wa Kizayuni wa Israel kuwa utawala wa kigaidi.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya Vibonzo ya Amerika ya Latini hapa mjini Tehran, Alberto Gonzalez Casals, Balozi wa Cuba nchini Iran amesema Israel ni dola la kigaidi, licha ya utawala huo haramu kuitaja Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwa kundi la kigaidi.

Amebainisha kuwa, "Israel inaiita HAMAS kuwa ni kundi la kigaidi, na Wamagharibi wakiongozwa na Marekani wanaitazama HAMAS kama kundi la kigaidi, lakini wao wenyewe ndio magaidi halisi."

Kadhalika amezitaka nchi za Magharibi ziache kuikingia kifua Israel na kuzuia hatua yoyote ya kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni unaoendelea kukiuka sheria za kimataifa.

Jinai za Israel katikak Ukanda wa Gaza

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Cuba amelaani vikali mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambayo mpaka sasa yameua shahidi Wapalestina zaidi ya 9,000.

Hivi karibuni, Kamisheni ya Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge la Cuba ililaani jinai na mashambulio ya kikatili yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na hatia wa Palestina, na kuitaka Israel ikomeshe ukatili wake huo.

Kabla ya hapo pia, mamia ya maelfu ya wananchi wa nchi nyingine ya Amerika ya Latini ya Chile walikuwa wamendamana kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina.

Tags