Nov 24, 2023 07:21 UTC
  • Russia yataka kurejea Marekani na Troika ya Ulaya kwenye makubaliano ya nyuklia na Iran

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika taasisi za kimataifa ameeleza kuwa, Moscow inazitaka Marekani na kundi la Troika ya Ulaya zirejee katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran.

Mikhail Ulyanov Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Russia amesema katika mkutano wa Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia kuwa: Tunaiomba Marekani na nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza (kwa jina la Troika ya Ulaya) zitilie mkazo  kufufua mapatano ya JCPOA badala ya kujaribu kuvuruga au kukwamisha ushirikiano kati ya Iran na Wakala IAEA. 

Makubaliano ya JCPOA 

Troika ya Ulaya jana Alhamisi ilitoa taarifa ya pamoja katikakikao cha Bodi ya Magavana ya IAEA na baada ya kukariri madai na tuhuma mbalimbali dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani zilidai kuwa zina nia ya kupata ufumbuzi wa kidiplomasia ili kutatua shaka zilizopo kuhusu shughuli za nyuklia za Iran.  

Wakati huo huo Amir Saeed Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa hivi karibuni alijibu barua ya wawakilishi wa Troika ya Ulaya katika Umoja wa Mataifa kwa kusema: Wawakilishi wa kudumu wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza katika Umoja wa Mataifa Novemba 14 mwaka huu walitoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran na kudai kuwa Iran imekiuka azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la UN la mwaka 2015; huku nchi hizo zikipuuza kukiuka waziwazi azimio hilo. 

 

Tags