M’membe: Vikwazo vya Magharibi vimezikurubisha pamoja Russia, Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i106410-m’membe_vikwazo_vya_magharibi_vimezikurubisha_pamoja_russia_afrika
Rais wa Chama cha Kisoshalisti cha Zambia amesema nchi za Magharibi zinaziburuza nchi nyingine duniani kuingia vitani huku zikipora rasilimali zao.
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
Dec 25, 2023 10:42 UTC
  • M’membe: Vikwazo vya Magharibi vimezikurubisha pamoja Russia, Afrika

Rais wa Chama cha Kisoshalisti cha Zambia amesema nchi za Magharibi zinaziburuza nchi nyingine duniani kuingia vitani huku zikipora rasilimali zao.

Fred M’membe amesema hayo katika mahojiano na kanali ya Russia Today na kuongeza kuwa, Marekani na Ulaya zinafanya hima kuimarisha ubeberu wao kwa upande mmoja, na kuiba rasilimali za mataifa mengine kwa upande mwingine.

Mwanasiasa huyo wa Zambia ameeleza bayana kuwa, "Wamagharibi wanazisukuma nchi nyingine ziingie vitani. Wanapora rasilimali za mataifa mengine."

Ameashiria pandekezo la Rais Joe Biden wa Marekani la kuhamishiwa Ukraine mali za Russia zilizozuia kutokana na vikwazo US na Ulaya na kusisitiza kuwa, viongozi wa Magharibi wana maradhi na uchu wa kupora mali na rasilimali za wengine bila mipaka yoyote.

Rais Vladimir Putin wa Russia alipokutana na viongozi wa Afrika

Rais wa Chama cha Kisoshalisti cha Zambia amewahutubu watawala wa Magharibi kwa kusema: Hawa ni wezi, wakiwa na mgogoro, wanageukia wizi. Wanaiba rasilimali za dunia.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo wa Zambia, vikwazo vya Magharibi kinyume na matarajio yao, imekuwa chachu ya kupangua na kupanga upya siasa za dunia, jambo ambalo limepelekea kuimarika uhusiano na ushirikiaino baina ya Russia na mataifa ya Afrika.

M'membe ameongeza kuwa, umoja na ushirikiano wa Russia na Afrika hivi sasa umerejea katika kiwango cha juu, kama ilivyoshuhudiwa kabla ya kuanguka Umoja wa Sovieti.