Russia yalaani NATO kujipania kuelekea Mashariki
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10996-russia_yalaani_nato_kujipania_kuelekea_mashariki
Russia imelaani vikali hatua ya muungano wa kijeshi wa NATO kujipanua na kuelekeza nguvu zake Moscow wakati ambapo hakuna tishio lolote kutoka mashariki.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 10, 2016 14:37 UTC
  • Russia yalaani NATO kujipania kuelekea Mashariki

Russia imelaani vikali hatua ya muungano wa kijeshi wa NATO kujipanua na kuelekeza nguvu zake Moscow wakati ambapo hakuna tishio lolote kutoka mashariki.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa leo Jumapili na kusema: "Kinyume na lengo lake la kudumisha Amani na uthabiti Ulaya…NATO inajikita katika kuzuia tishio ambalo haliko kutoka Mashariki."

Taarifa hiyo imesema mkutano wa viongozi wa NATO uliomalizika Jumamosi huko Warsaw Poland ulitilia mkazo tishio bandia kutoka Russia.

Viongozi wa nchi 28 wanachama wa muungano wa kijeshi wa NATO waliafiki kuhuisha jumuiya hiyo ya kijeshi ili kukabiliana na kile walichodai kuwa ni tishio kutoka Russia.

Uhusiano baina ya Russia na NATO ulizorota miaka miwili iliyopita kutokana na mgogoro wa Ukraine ambapo nchi za Magharibi zinadai kuwa Moscow ilihusika katika uasi mashariki mwa nchi hiyo. Wakuu wa Russia wamekanusha vikali madai hayo.

Russia pia imekosoa kuzidi kupanuka NATO na kuzijumuisha nchi za eneo la Magharibi mwa Balkan na kusema hatua hiyo inahatarisha maslahi yake ya kistratijia katika eneo hilo.

Mkutano huo wa NATO mjini Warsaw alifanyika chini ya ulinzi mkali ambapo kuliwa na wanajeshi 6000 waliokuwa na jukumu la kuwalinda wajumbe 2000 walioshiriki katika kikao hicho.

Aidha mamia ya waandamanaji wanaopinga vita walijumuika mjini humo kulalamikia hatua za kijipanua zaidi NATO na namna muungano huo unaovyeneza sera za kivita duniani.