Apr 29, 2024 02:36 UTC
  • Intelijinsia Marekani: Putin hakuamuru kuuliwa Navalny

Jarida la Wall Street limezinukuu duru za kiintelijinsia za Marekani na kuripoti kuwa Rais Vladmir Putin wa Russia hakuagiza kuuawa mwanasiasa wa upinzani wa nchi hiyo, Alexei Navalny, aliyefia gerezani mwezi Februari mwaka huu.

Ripoti hii iliyotolewa kwa kuzinukuu duru za kijasusi za Marekani imeeleza kuwa, uchunguzi umefanywa ili kubainiki sababu ya kifo chache. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, CIA, Kurugenzi ya Kitaifa ya Ujasusi na Idara ya Ujasusi ya Usalama wa Ndani ya Marekani pia zimeidhinisha maoni ya yaliyotolewa na duru za ujasusi za nchi hiyo. 

Chanzo cha kifo cha Navalny bado hakijajulikana kutokana na hali ambazo hazijafafanuliwa kutoka kwenye vyanzo vya habari. Viongozi wengi wa nchi za Ulaya na Rais Joe Biden wa Marekani walimtuhumu Rais Putin kuwa amehusika na kifo cha mwanasiasa huyo wa upinzani alifariki dunia akiwa jela mnamo Februari 16 mwaka huu. 

Rais Vladimir Putin wa Russia 

Rais wa Marekani alisema baada ya kuaga dunia mwanasiasa huyo wa upinzani wa Russia kwamba: "usifanye makosa, Putin anahusika na kifo cha Navalny."  

Alexei Navalny alikamatwa na kutiwa nguvuni katika uwanja wa ndege wa Moscow mwezi Januari mwaka 20211 wakati akirejea katika mji mkuu huo wa Russia baada ya kutoka matibabuni huko Berlin, Ujerumani. Alikwenda Ujerumani kwa matibabu kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alipewa sumu. 

Mwezi Agosti mwaka jana, mahakama ya Russia ilimhukumu  Navalny kifungo cha miaka 19 jela kwa kosa la kausisi kundi lenye misimamo mikali akiwa gerezani. 

Tags