Unyanyasaji wa kijinsia waongezeka katika shule za Uingereza
Utafiti wa pamoja wa Muungano wa wafanyakazi wa kielimu, "Unison" na "UK Feminista" nchini Uingereza unaonyesha kuwa robo ya wafanyakazi wa shule za upili katika nchi hiyo wameshuhudia unyanyasaji wa kijinsia katika mazingira ya shule hizo, katika miaka 5 iliyopita.
Kulingana na shirika la habari la IRIB, uchunguzi huu umethibitisha ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia katika shule za Uingereza, ukitoa mfano wa wafanyakazi wa kike katika shule za upili za Uingereza ambao mara kwa mara wamekuwa walengwa wa unyanyasaji wa kijinsia na wanafunzi wa kiume au wafanyakazi wa shule ya watoto wa kiume.
Katika uchunguzi huu, asilimia 10 ya wafanyakazi wa shule za upili za Uingereza walisema kuwa katika miaka 5 iliyopita, wao wenyewe wamenyanyaswa kijinsia katika maeneo ya kazini.
Jarida la The Guardian liliandika kuhusu suala hili likiisema: Asilimia 7 ya wafanyakazi wa kike katika shule za msingi na sekondari za Uingereza wanasema wanasumbuliwa na unyanyasaji wa kijinsia mara kwa mara.
Takwimu hizi zinatolewa huku asilimia 42 ya wafanyakazi ambao wameshuhudia unyanyasaji wa kijinsia katika shule za Uingereza wanasema kwamba hawakuripoti kesi hizo kwa sababu wanaona kuwa hatua hii haina faina faida kutokana na kutochukuliwa hatua za maana
Katika uchunguzi wa pamoja uliofanywa na Muungano wa wafanyakazi wa kielimu, "Unison" na "UK Feminista" nchini Uingereza ambao ulifanyika Machi 20 hadi 29 mwaka huu, asilimia 49 ya wafanyakazi wa shule za sekondari, na asilimia 31 ya wafanyakazi wa shule za msingi, na asilimia 9 ya walimu wa shule za chekechea na asilimia 8 ya wafanyakazi wa shule maalumu, asilimia mbili ya wafanyakazi wa shule zenye idara zote mbili za msingi na sekondari na asilimia moja ya wafanyakazi wa idara maalumu za watoto wenye mahitaji maalumu walishiriki.