Rais Sally: Waislamu ni wahanga wakubwa wa ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11422-rais_sally_waislamu_ni_wahanga_wakubwa_wa_ugaidi
Rais wa Senegal amesema kuwa Waislamu ni wahanga wakubwa wa ugaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 17, 2016 08:06 UTC
  • Rais Sally: Waislamu ni wahanga wakubwa wa ugaidi

Rais wa Senegal amesema kuwa Waislamu ni wahanga wakubwa wa ugaidi duniani.

Akizungumza katika mahojiano na kanali ya televisheni ya France 24, Rais Mack Sally amesema kuwa nchi za Kiislamu ni wahanga wakubwa wa ugaidi duniani. Rais wa Senegal ameongeza kuwa nchi zote duniani zinapasa kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi na kwamba kinyume na hivyo, ulimwengu kwa mara nyingine tena utashuhudia matukio kama lile lililotokea katika mji wa Nice kaskazini mwa Ufaransa.

Watu 84 waliuawa na wengine 200 kujeruhiwa Alhamisi iliyopita katika shambulio la kigaidi lililofanywa na mtu mmoja aliyeendesha gari na kuukanya umati mkubwa wa watu waliokuwa katika sherehe za kitaifa za Siku ya Bastille katika mji wa Nice.

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na shambulio hilo la kinyama huko Ufaransa.