Mauaji ya kimbari ya Israel yalaaniwa katika Bunge la Ubelgiji
Mwakilishi wa Bunge la Ubelgiji amelaani hadharani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Gaza.
Nabil Boukili, mwakilishi katika Bunge la Ubelgiji amesema: Suala muhimu na la msingi ni kuuadhibu utawala wa Israel unaofanya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza. Kwa nini tumeuacha na na kuutouwekea vikwazo utawala unaofanya mauaji ya halaiki kwa makumi ya mara bali kwa zaidi ya mamia?
Mbunge huyo wa Ubelgiji amemhutubia Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kusema: Miili ya zaidi ya watu 300 imegunduliwa katika kaburi la pamoja katika hospitali ya Khan Yunis katika Ukanda wa Gaza. Pia, miili ya zaidi ya watu 380 iligunduliwa katika hospitali ya al-Shifa baada ya wanajeshi wa jeshi la Israel kuondoka hospitalini.
Huku akikumbusha jinai za utawala wa Kizayuni, mbunge huyo wa Ubelgiji amesema: "Mifereji na mitaro iliyojaa maiti za watu, je, haikukumbushi mauaji ya umati ambayo tuliyashuhudia katika historia yetu?"
Mbunge huyo wa Bunge la Ubelgiji amekosoa kutoonyesha hisia nchi za Ulaya kwa jinai za Wazayuni, na kuongeza kuwa: "Uhalifu unafanywa mbele ya macho yetu, lakini je, hazipaswi kuchukuliwa hatua za kuuzuia utawala ghasibu wa Israel unaofanya jinai za mauaji ya umati?" Hii ni tabia ya kinafiki isiyoelezeka.
Mwakilishi huyu wa bunge la Ubelgiji amesema kuhusu kuitambua nchi Palestina: Huku ni kuheshimu tu sheria za kimataifa lakini hakuna utekelezaji wa kivitendo. Tunafanya hivi ili kuepuka kupiga kura juu ya suala muhimu zaidi na la kweli la kuadhibu Israel.