Waislamu wa Hamburg watekeleza Swala barabarani wakipinga kufungwa msikiti wao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i114774-waislamu_wa_hamburg_watekeleza_swala_barabarani_wakipinga_kufungwa_msikiti_wao
Waislamu wa Hamburg nchini Ujerumani jana walikusanyika na kuswali barabarabi mbele ya Msikiti Imam Ali wakilalamikia ukandamizaji dhidi ya jamii za Kiislamu.
(last modified 2024-08-03T00:57:34+00:00 )
Aug 03, 2024 00:57 UTC
  • Waislamu wa Hamburg watekeleza Swala barabarani wakipinga kufungwa msikiti wao

Waislamu wa Hamburg nchini Ujerumani jana walikusanyika na kuswali barabarabi mbele ya Msikiti Imam Ali wakilalamikia ukandamizaji dhidi ya jamii za Kiislamu.

Waislamu hao wamelazimika kuswalia barabarani baada ya serikali ya Ujerumani kufunga Msikiti wa Iman Ali na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg huko Kaskazini mwa Ujerumani.

Polisi ya Ujerumani ilivamia na kupekuua Kituo cha Kiislamu cha Hamburg na vituo kadhaa tanzu yakiwemo majengo 53 katika mikoa 8 ya Ujerumani. 

Baada ya hatua hiyo, serikali ya Ujerumani ilipiga marufuku shughuli za Kituo cha Kiislamu cha Hamburg na mashirika yake yote katika nchi hiyo. 

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amelaani vikali hatua ya polisi ya Ujerumani ya kupiga marufuku Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) na asasi zake tanzu, na kusema kwamba hatua hiyo inakiuka kanuni za kimsingi za uhuru wa kuabudu.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wa X,  amesema  kuwa hatua hiyo ni zawadi kwa watu wenye itikadi kali, watu wanaochochea ghasia na watetezi wa ugaidi.

Bagheri Kani aliongeza: "Utawala wa kigaidi wa Israel, ambao unatumia kila kisingizio kugeuza maoni ya umma kutoka kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya Wapalestina, pia uliunga mkono hatua ya polisi wa Ujerumani."

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani ilidai kwamba "imepiga marufuku Kituo cha Kiislamu cha Hamburg na mashirika yake tanzu kote Ujerumani kwa madai kuwa eti ni taasisi yenye itikadi kali la Kiislamu."