Ban atoa wito wa kuzuiwa hujuma dhidi ya Uislamu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba vitendo vya hujuma dhidi ya wageni, propaganda chafu dhidi ya Uislamu na mivutano ya kikaumu na kimadhehebu vimeongeseka kote duniani na kuogeza kuwa kutolewa elimu sahihi ndiyo ufunguo wa matatizo hayo yote.
Ban Ki-Moon amesema njia yenye taathira kubwa zaidi katika kulinda haki za wanadamu, kukabiliana na hujuma dhidi ya wageni na mauaji ya kimbari ni kutolewa mafunzo sahihi na ya dharura kwa vizazi vipya. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa walimwengu wanawajibika kufanya jitihada kubwa za kutetea haki za binadamu kwa kutilia maanani ongezeko kubwa la wimbi la fikra mbalimbali, matamshi yanayohujumu Uislamu na ubaguzi wa aina mbalimbali.
katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria pia jinai zinazofanywa na kundi la Daesh dhidi ya makundi ya dini za waliowachache na mgogoro wa Syria ambao umesababisha mgogoro mkubwa wa binadamu na kusema, kuna udharura wa kuheshimiwa itikadi na imani za makundi na watu mbalimbali.