Bulgaria yapiga marufuku 'propaganda' za kueneza 'Ushoga' katika skuli na vituo vya malezi ya watoto
Bunge la Bulgaria limeidhinisha marekebisho ya Sheria ya Taifa ya Elimu ambayo yatapiga marufuku ushajiishaji wa mahusiano ya kingono "yasiyo ya jadi" pamoja na kubadilisha kijinsia, katika maskuli na vituo vya malezi ya watoto.
Mswada huo ulipitishwa siku ya Jumatano baada ya kusomwa mara mbili kufuatia masaa manne ya majadiliano makali. Baada ya kusomwa mara ya pili na ya mwisho, wabunge 135 waliunga mkono sheria hiyo huku 57 wakipiga kura dhidi yake na wanane kuamua kutopiga kura.
Marekebisho hayo yaliyowasilishwa na Chama cha Uamsho chenye mielekeo ya utaifa, yaliidhinishwa na vyama vingi katika Bunge, ikiwa ni pamoja na GERB-SDS cha katikati-kulia, Chama cha Kisoshalisti cha Bulgaria cha mrengo wa kushoto na wanachama wengi wa DPS wenye msimamo mkali.
Kiongozi wa Chama cha Uamsho Kostadin Kostadinov amesisitiza kuwa itikadi ya LGBT "si ya ubinadamu" na inapiga vita utu kwa kushajiisha "mahusiano yasiyo ya jadi" maskulini.../