Wananchi wa Ireland wataka kukomeshwa ukoloni wa Uingereza nchini mwao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i119834-wananchi_wa_ireland_wataka_kukomeshwa_ukoloni_wa_uingereza_nchini_mwao
Wananchi wa Ireland kwa mara nyingine tena wametoa mwito wa kukomeshwa utawala wa Waingereza huko Ireland Kaskazini. Hayo yamekuja wakati Ireland ikiadhimisha kuanzishwa Jimbo Huru la Ireland ambalo linajumuisha kaunti 26 za Jamhuri ya Ireland. Hivi sasa kuna Kaunti sita za Jamhuri ya Ireland bado ziko chini ya udhibiti wa nchi ya kifalme ya Uingereza.
(last modified 2024-12-07T08:06:48+00:00 )
Dec 07, 2024 08:06 UTC
  • Wananchi wa Ireland wataka kukomeshwa ukoloni wa Uingereza nchini mwao

Wananchi wa Ireland kwa mara nyingine tena wametoa mwito wa kukomeshwa utawala wa Waingereza huko Ireland Kaskazini. Hayo yamekuja wakati Ireland ikiadhimisha kuanzishwa Jimbo Huru la Ireland ambalo linajumuisha kaunti 26 za Jamhuri ya Ireland. Hivi sasa kuna Kaunti sita za Jamhuri ya Ireland bado ziko chini ya udhibiti wa nchi ya kifalme ya Uingereza.

Tarehe 6 Disemba ambayo mwaka huu ilikuwa ni jana Ijumaa, ni kumbukumbu ya kuanzishwa Jimbo Huru la Ireland mwaka 1922 lakini licha ya kupita zaidi ya karne moja, bado kuna ardhi za Jamhuri ya Ireland hazijakombolewa.

Utawala wa kifalme wa Uingereza ulifanya jinai kubwa katika kipindi ambacho ni maarufu kwa jina la 'The Troubles' ambacho kiligubikwa na ukatili mwingi uliofanywa na wanajeshi hao vamizi wa Uingereza.

Kwa mfano, mwaka 1972 Jeshi la Uingereza liliwapiga risasi raia 26 wasio na silaha wakati wa maandamano yaliyofanyika Derry's Bogside. Wakatoliki 14 wasio na hatia waliuliwa kwa damu baridi kabisa na wanajeshi vamizi wa Uingereza.

Ukatili wa Uingereza kwa Wakatoliki na wananchi wa Ireland ni mkubwa. Hii ni picha ya kihistoria ya maziko ya wananchi wa Ireland waliouliwa na wanajeshi wa Uingereza

 

Kwa mujibu wa Press TV, historia ya umwagaji damu ya wanajeshi wa Uingereza huko Ireland Kaskazini ni ya kutisha kutokana na kuua kikatili Wakatoliki wengi bila ya kosa lolote.

Kovu la ukatili huo lipo hadi leo na inaonekana litabakia milele. Mwaka 1972 wanajeshi wa Uingereza walifanya shambulio baya zaidi katika historia ya Ireland Kaskazini kwa kuwapiga risasi wananchi wasio na hatia na kuzidisha moto wa vita. 

Raia mmoja wa Jamhuri ya Ireland ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 72 amenukuliwa akisema: "Nimeshuhudia mauaji ya watu mitaani na damu zikitiririka barabarani. Nilikuwa pamoja na watu waliouwa kwa kupigwa risasi kando yangu, karibu sana na mimi kama nilivyo karibu na wewe hivi sasa, na damu zao zilinirukia mimi, na sote tulikuwa tukingoja kuuliwa kikatili na wanajeshi hao wa Uingereza.