WHO yachunguza ugonjwa usiojulikana DRC
https://parstoday.ir/sw/news/world-i119914-who_yachunguza_ugonjwa_usiojulikana_drc
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kwamba linaendeleza uchunguzi kuhusu mripuko wa ugonjwa usiojulikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umeua idadi kubwa ya watu.
(last modified 2024-12-09T04:39:46+00:00 )
Dec 09, 2024 04:39 UTC
  • WHO yachunguza ugonjwa usiojulikana DRC

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kwamba linaendeleza uchunguzi kuhusu mripuko wa ugonjwa usiojulikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umeua idadi kubwa ya watu.

Katika mkoa wa Panzi, ulioko zaidi ya kilomita 700 kutoka mji mkuu Kinshasa, maambukizi 406 yameripotiwa na vifo 31. Wizara ya Afya ya Kongo imeripoti vifo vya ziada vilivyotokea nje ya vituo vya afya ambavyo vinavyohitaji kuchunguzwa na kuthibitishwa.

WHO imesema katika taarifa yake kuwa visa vingi vimevyoripotiwa miongoni mwa watoto, hasa wale walio chini ya umri wa miaka mitano, huku dalili za ugonjwa huo ambao hadi sasa haujajulikana ikiwa ni homa kali, mafua na matatizo ya kupumua. Magonjwa kama malaria, nimonia, COVID-19 na utapiamlo yanachangia kuibuka ugonjwa huo.

Waziri wa Afya Samuel Kamba Roger amesema kuwa serikali imetuma timu ya wataalam wa magonjwa ya milipuko ili kutathmini hali na kujua asili ya ugonjwa huo.